Hata na mgeni naye, asiyekuwa mmoja wa watu wako Israeli, atakapokuja kutoka nchi iliyo mbali sana kwa ajili ya jina lako kuu, na mkono wako ulio hodari, na mkono wako ulionyoshwa; hao watakapokuja na kuomba wakiielekea nyumba hii; 2 Wafalme 6:32.

Thursday, 6 March 2014

Obama awasiliana na Putin kuhusu Ukraine

rtx10r8d.si_49338.jpg
Rais Obama amefanya mazungumzo zaidi ya kina na rais wa Urusi Vladmir Putin akisistiza kuwa vitendo vya nchi yake katika jimbo la Crimea ni ukiukaji wa mipaka na uhuru wa taifa la Ukraine.
Wakati wa mazungumzo yao ya pili kupitia njia ya simu katika kipindi cha siku sita zilizopita, bwana Obama amependekeza njia ya kusuluhisha mzozo huo kidiplomasia inayojumuisha Urusi kuwaondoa wanajeshi wake katika jimbo la Crimea. Bwana Putin amesema uhusiano kati ya Moscow na Washington haufai kutatizika kutokana na mzozo wa Ukraine.
Awali bwana alisema kuwa kura ya maoni iliyopendekezwa kuhusu jimbo la Crimea kujiunga na Moscow inakiuka sheria ya kimataifa na sharti ijumuishe serikali ya Kiev iwapo itaandaliwa.
Akizungumza baada ya mkutano mwingine wa Baraza la Usalama uliofanyika faraghani, balozi wa Uingireza katika umoja wa mataifa , Mark Lyall Grant, amesema haiwezekani muafaka kupatikana katika baraza hilo kuhusu mzozo huo.
"Nadhani hakuna dalili kwamba kutakuwa na mwafaka katika baraza la usalama katika kipindi cha siku chache zijazo. Kama ulivyosikia kutoka kwa wengine, kuna mashauri yanayoendelea kati ya wanadiplomasia kwenye mikutano mbali mbali Ulaya. Mashauri hayo yataendelea,'' amesema bwana Grant.
''Pengine kiwango fulani cha makubaliano kitaafikiwa ili kutuliza mgogoro huu na kisha baraza la usalama pengine litapata suluhu. Lakini hatujafutilia mbali mpango wa kuwasilisha azimio mbele ya Baraza la Usalama wakati wowote na tunafuatilia hali ya mambo kwa karibu tukitarajia baraza la Usalama likutane tena katika siku chache zijazo ikitegemea kitakachotokea mashinani."
Mzozo huo wa Ukraine umechochea wanasiasa pamoja na wageni wengine mashuhuri kususia mashindano ya Olimpiki ya wanariadha walemavu nchini Urusi. Marekani imeondoa ujumbe wake katika michezo hiyo na mawaziri wa Uingereza hawatakuwepo sawia na wenzao kutoka mataifa mengine ya Ulaya.(P.T)

No comments: