TP Mazembe walishindi mahasidi wao wa jadi AS Vita
kutoka Jamhuri ya Kidemkrasia ya Congo katika mechi iliyobashiriwa kuwa
ngumu ya kundi A ya kuwania ubingwa wa Afrika miongoni mwa vilabu .
Mechi hiyo ya Jumapili ilichezwa katika hali ya
taharuki kufuatia matukio yaliyopelekea kufa kwa mashabiki 15 katika
uwanja wa Tata Raphael ulioko Kinshasa yapata majuma mawili yaliyopita
timu hizo zilipokutana katika mechi ya ligi ya nyumbani.TP Mazembe walishinda mechi hiyo kwa bao 1-0.
Kufikia sasa timu zote zilizo katika kundi A zimeshinda mechi moja moja baada ya klabu ya Misri, Zamalek, kuishinda Al Hilal ya Sudan jijini Kairo na kunyakua pointi 3.
Ahly iliilaza Esperance ingawa walipoteza kwa kutocheza mechi yao ya nyumbani kufuatia machafuko ya wafanyikazi katika mji upatikanao katika pwani ya Tunisia, Sfax.
No comments:
Post a Comment