Apostle Livingstone Banjagala akiwa anatoa Unabii
Siri Nzito kuhusiana na Mapepo wachafu ilifichuliwa jumapili katika kanisa la moja lijulikanalo kwa jina la City Harvest Internationa Church lililoko maeneo ya Posta mpya Jengo la jubilee tower Gorofa ya nne. Chanzo chetu kilipowahoji baadhi ya washirika hao walisema kweli mapepo hayatawahi kuwachezea tena maana wamejua siri, wengi wao walionekana na nyuso za furaha kwani walikuwa wameteswa na mapepo kwa muda mrefu sana na wengine hawakuweza kujielezea ila kuishia kuseama tu "ASANTE YESU" kwa furaha. Juhudi za kuongea na Nabii huyo (Apostle Livingstone) ziliambulia patupu na pia tulijaribu kumpigia simu yake ya mkononi lakini haikupokelewa ila tulifanikiwa kuongea na Mchungaji msaidizi wa kanisa hilo ambaye hakupenda jina lake litajwe na alituambia kuwa Nabii huyo amekuwa akiachia unabii mzito juu ya watu na kuombea wagonjwa na wenye matatizo sugu mpaka mara nyingine walishangazwa na nguvu za Mungu ambazo zimekuwa zikizoshuka mahali hapo na kusema hakika kweli Mungu yupo.
No comments:
Post a Comment