Wagombea wakuu wa uchaguzi nchini Nigeria rais Goodluck Jonathan wa Nigeria na Muhammud Buhari
Wagombea wawili wa uchaguzi wa urais nchini Nigeria wameahidi kufanyika kwa uchaguzi wa amani,na kuongezea kuwa wataheshimu matokeo ya uchaguzi ulio huru na haki.
Rais Goodluck Jonathan pamoja na mpinzani wake wa karibu Muhammadu Buhari,pia wamewataka wafuasi wao kuiga mfano huo.
Uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika siku ya jumamosi baada ya kuahirishwa mwezi uliopita.
Mwandishi wa BBC amesema kuna wasiwasi kuhusu iwapo tume ya uchaguzi imejianda kusimamia uchaguzi huo na iwapo shughuli hiyo itaafikia matarajio ya wengi.
No comments:
Post a Comment