Hata na mgeni naye, asiyekuwa mmoja wa watu wako Israeli, atakapokuja kutoka nchi iliyo mbali sana kwa ajili ya jina lako kuu, na mkono wako ulio hodari, na mkono wako ulionyoshwa; hao watakapokuja na kuomba wakiielekea nyumba hii; 2 Wafalme 6:32.

Saturday, 28 March 2015

Makabiliano Hotelini Somalia yamalizika


Makabiliano kati ya vikosi vya serikali na wapiganaji wa Al Shabaab katika hoteli ya Al Mukarama yamemalizwa kwa mujibu wa maafisa wa serikali ya Somalia

Maafisa wa serikali ya Somalia wanasema kuwa mapigano yalikuwa kwenye hoteli moja mjini Mogadishu kufuatia uvamizi wa wanamgambo wa Al shabaab yamemalizika.

Maafisa hao walisema kuwa wanajeshi wa serikali waliingia eneo hilo kuidhibiti hoteli ya Maka al Mukarama zaid ya saa 12 baada ya wanamgambo kuivamia.
Watu 9 waliuwa wakati wa uvamizi huo akiwemo mjumbe mmoja wa Somalia.
Waandishi wa habari eneo hilo wanasema kuwa miili ya wanamgambo na ya wanajeshi ilikuwa eneo hilo.
Wataalamu wa kutegua mabomu wanasaka hoteli hiyo kujua iwapo kuna milipuko yoyote.

No comments: