Saturday, 28 March 2015
Mtandao wa tume ya uchaguzi Nigeria warekebishwa
Hatimaye mtandao wa tume ya uchaguzi nchini Nigeria umeanza tena kufanya kazi
Mtandao wa tume ya uchaguzi nchni NIgeria INEC ambao ulikuwa umeingiliwa na kundi la wahalifu wa mtandao linalojiita jeshi la mtandaoni la Nigeria hatimaye umeanza tena kufanya kazi.
Kundi hilo linalojiita Jeshi la mtandaoni la Nigeria liliweka ujumbe katika tovuti hiyo likiionya tume ya uchaguzi ya Nigeria dhidi ya kufanya udanganyifu katika uchaguzi huo.
kufikia sasa haijulikani iwapo wahalifu hao wameingia zaidi ya mtandao huo ijapokuwa wamesema kuwa walikuwa wakithibiti data yote ya tume ya uchaguzi.
Tume hiyo imesema kuwa ina maelezo kuhusu shambulizi hilo la mtandaoni na sasa imeanza kufanya uchunguzi.
Ujumbe huo wa wahalifu hao wa mtandaoni pia unasema kuwa wameweza kuingilia data ya serikali.
Mitandao kadhaa maarufu ya serikali ya Nigeria imefungwa katika miaka ya hivi karibuni ukiwemo ule wa bunge.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment