Mtandao wa tume ya uchaguzi nchini Nigeria waingiliwa
Huku mamilioni ya raia wa Nigeria wakipiga kura kumchagua rais mpya,tovuti ya tume ya uchaguzi nchini Nigeria imeingiliwa na wahalifu wa mtandaoni.
Kundi linalojiita Jeshi la mtandaoni la Nigeria limeweka ujumbe katika tovuti hiyo likiionya tume ya uchaguzi ya Nigeria dhidi ya kufanya udanganyifu katika uchaguzi huo.
kufikia sasa haijulikani iwapo wahalifu hao wameingia zaidi ya mtandao huo ijapokuwa wamesema kuwa walikuwa wakithibiti data yote ya tume ya uchaguzi.
Tume hiyo imesema kuwa ina maelezo kuhusu shambulizi hilo la mtandaoni na sasa imeanza kufanya uchunguzi.
Ujumbe huo wa wahalifu hao wa mtandaoni pia unasema kuwa wameweza kuingilia data ya serikali.
Mitandao kadhaa maarufu ya serikali ya Nigeria imefungwa katika miaka ya hivi karibuni ukiwemo ule wa bunge.
No comments:
Post a Comment