Wednesday, 9 November 2016
👩*KURUDISHA NAFASI YA MWANAMKE ILIYOPOTEA NDANI YA KANISA , FAMILIA NA TAIFA*👩
Na Bishop Dankton Rudovick Rwekila
Wakati tunarudisha nafasi ya mwanamke👩 kwenye familia👪, kanisa, taifa na Dunia🌍 kwa ujumla , ni muhimu kuweza kutambua ni nafasi ipi iliyopotea.
MOYO💖 WA USHAURI ULIOAMBATANA NA HEKIMA YA USHAURI
Mungu alimuumbia mwanamke Roho ya uvumilivu, Mwanamke akiliamini jambo na kulipenda anasimamia kwa nguvu zake zote. Mwanaume akipenda jambo anakuwa anachunguza chunguza. Ndiyo maana hata katika hali ya kanisa🏰 katika kububujika na kumpokea Roho Mtakatifu ni wanawake ndiyo wa kwanza , Hata wakati wa Bwana Yesu kwenda kumuona kaburini ( Mathayo 28:1)
Hawa👩 alikuwepo kwaajili ya ushauri kwa Adamu👷. Mwanamke aliporidhika na maelezo ya Nyoka🐍 moyo wake ukabadilika na akalipeleka kwa Mume wake
Shetani hali akijua nguvu iliyopo ndani ya mwanamke ya ushawishi ndiyo maana misuko suko mingi sana inawakuta wanawake. Shetani anajua nguvu ya ushawishi wa mwanamke, ndani ya familia👪 ndiyo maana anaweka uchungu mkubwa ndani ya moyo💖 wake na kutoa moyo wa ushauri ambao ndiyo asili lake.
Moyo wenye uchungu wa mwanamke utashauri, uchungu, mawazo yake binafsi, uchovu. 📖Biblia inasema kiujazacho 💖Moyo ndicho kimtokacho mtu ndicho kimeujaza moyo wake.
Mwanamke anaweze kusema jambo leo na wakati mwingine kwasababu ya 👷ubaba , Mwanamume anafanya kwa kuamrisha ila Mwanamke atahakikisha kile ambacho amekitaka kinakuwa vile vile hata baada ya miaka mitano👊, atatumia nguvu yake ya ushawishi na utakuta mwanaume akikubaliana naye baada ya Muda mfupi. Mara nyingi mwanaume jambo lake ni papo kwa papo. Mwanaume usahau mapema ila ni tofauti kwa mwanamke atalifanyia kazi jambo mpaka litimie.
Kwenye familia Mama akikupenda💝 hata Baba asipokupenda tambua kwamba ipo siku kutokana na ushawishi wa mama, Baba atakupenda tu kutokana na nguvu iliyopo ndani ya mwanamke , inayoambatana na moyo wa ushawishi. Mwanamke amepewa nafasi ya kubadili familia.👪
Mwanamke kwa nafasi aliyopewa ya Moyo wa ushauri unaweza kufungua baraka ndani ya Nyumba 🏡
📖_2 Wafalme 4:9-16 Yule mwanamke akamwambia mumewe, Tazama, mimi naona ya kuwa mtu huyu apitaye kwetu mara kwa mara ni mtu mtakatifu wa Mungu. Nakuomba, tumfanyie chumba kidogo ukutani; na ndani yake tumwekee kitanda, na meza, na kiti, na kinara cha taa; na itakuwa, atujiapo, ataingia humo. Ikawa siku moja akafika huko, akaingia katika chumba kile akalala. Akamwambia Gehazi mtumishi wake, Mwite yule Mshunami. Naye alipokwisha kuitwa, akasimama mbele yake. Akamwambia, Sema naye sasa, Tazama, wewe umetutunza sana namna hii; utendewe nini basi? Je! Uombewe neno kwa mfalme, au kwa amiri wa jeshi? Yule mwanamke akamjibu, Mimi ninakaa katika watu wangu mwenyewe. Akasema, Basi, atendewe nini? Gehazi akajibu, Hakika hana mwana, na mumewe ni mzee. Akamwambia, Kamwite. Naye alipokwisha kuitwa, akasimama mlangoni. Akasema, Panapo wakati huu mwakani, utamkumbatia mwana. Akasema, La! Bwana wangu, wewe mtu wa Mungu, usiniambie mimi mjakazi wako uongo.
Mwanamke huyu tunayemsoma📖 katika habari hii anamshauri mumewe kujenga chumba🏡 kwaajili ya watumishi wa Mungu ambao hata mume wake alikuwa awajui. Lakini kwasababu ya ushawishi na nguvu ya ushauri ya mwanamke malango ya Baraka yalifunguliwa ndani ya nyumba yao.
Mwanamke akimkaribisha mtu nyumbani mwake mwanaume awezi kukataa, lakini sivyo kwa kwa mwanaume , unaweza kutumia ubavu💪 lakini, kutokana na nguvu ya ushawishi na ushauri wa mwanamke mtu huyo ataondoka tu.
✔Mwanamke si mtawala lakini anayo mamlaka tena yenye nguvu. Ni sawa sawa na Rais, Bunge na Mahakama kila muhimili unamamlaka yake tena yenye nguvu. Ndiyo maana Biblia📖 inasema mwanamke mpumbavu uivunja nyumba yake kwa mikono yake mwenyewe.
Mfano wa Esta
Esta 5:1-8
Ikawa siku ya tatu Esta alijivika mavazi yake ya kifalme, akasimama katika ua wa ndani wa nyumba ya mfalme, kuielekea nyumba ya mfalme; naye mfalme akaketi juu ya kiti chake cha enzi katika nyumba ya mfalme, kuuelekea mlango wa nyumba. Ikawa, mfalme alipomwona malkia Esta amesimama uani, yeye akapata kibali machoni pake; naye mfalme akamnyoshea Esta fimbo ya dhahabu aliyokuwa nayo mkononi. Basi Esta akakaribia, akaigusa ncha ya fimbo.Mfalme akamwambia, Malkia Esta, wataka nini? Nayo ni haja gani uliyo nayo? Utapewa hata nusu ya ufalme. Esta akasema, Mfalme akiona vema, na aje leo, mfalme na Hamani, kwenye karamu niliyomwandalia. Basi mfalme akasema, Mhimize Hamani, ili ifanyike kama Esta alivyosema. Hivyo mfalme na Hamani wakafika katika karamu ile aliyoiandaa Esta.
Basi mfalme akamwambia Esta pale penye karamu ya divai, Dua yako ni nini? Nawe utapewa; na haja yako ni nini? Hata nusu ya ufalme utafanyiziwa. Esta akajibu, na kusema, Dua yangu ni hii, na haja yangu ni hii, Ikiwa nimepata kibali machoni pa mfalme, na mfalme akiona vema kunipa niombalo, na kunifanyizia haja yangu, na aje tena mfalme na Hamani kwenye karamu nitakayowaandalia, nami kesho nitafanya kama vile mfalme alivyosema.
Unaposoma Mistari ya hapo ☝juu na ukiangalia yale ambayo Esta alitaka kumuambia Mfalme utagundua Esta alikuwa na Siri nzito sana ndani ya Moyo💖 wake. Hata wakati anamkaribisha mume wake kwenye chakula🍝 na kwasababu ya nguvu ya ushawishi alimshawishi aje na Hamani .
Jambo kubwa ambalo lazima uone kwa macho tofauti ni pale mfalme alipomwambia Esta hata nusu ya ufalme💔 wake atampa, lakini Esta alikuwa na jambo lake ambalo aliitaji bado kulipika ndani ya moyo wa Mfalme . Unapoendelea na Mlango ule wa Saba utaona ombi la Malkia Esta . Kumbuka jambo moja Esta hakuwa mke pekee wa mfalme , Mfalme alikuwa na wake wengi na unaweza kufikiri kama angetoa nusu ya ufalme wake kwa Esta ambaye hakuwa na tamaa ya ufalme hao wengine wangekuwa katika hali gani.
Kupitia huu mfano wa Esta nataka nikuambie Siri ambayo makahaba wengi wanatumia kwaajili ya kuteka ndoa nyingi za wakristo. Mwanaume anarudi nyumbani akiwa mchovu na shughuli z hapa na pale, anamkuta mke Nyumbani badala ya kupokelewa na tabasamu anapokelewa na maneno ( Mimi nayaita mafaili) Mke anafungua faili la kila aina badala ya faraja na kubembelezwa huyu mwanaume tena aliyeokoka, anapokelewa kwa staili hiyo, Na Mwanaume wakati huo unahitaji kupembelezwa ili kesho unapoamka anakuwa na nguvu mpya kwasababu yupo mshauri ambaye amesimama katika nafasi yake. Anaitaji maneno matamu kama “Pole kwa kazi mume wangu, najua umechoka na kazi na najua pia changamoto za kazi/ Huduma ni nyingi sana lakini usijali mimi niko upande wako aijalishi hata kama unasemwa vibaya mimi niko upande wako, hata kama aujapata leo najua kesho utapata mume wangu, Mungu yupo upande wetu usiofu kabisa“ Sasa haya ni maneno baadhi tu yapo mengi mno ambayo hakika yanapotumika mtu usahahu kabisa kama alikuwa na changamoto za hapa na pale kwenye huduma au kwenye jambo lolote analolifanya kwa kusudi la Mungu. Lakini mtu huyu akafika nyumbani na kukutana na mafaili na anapokelewa nayo alafau kesho yake akutane na mtu anayejua kubembeleza hakika hii ndoa ya Kikristo tunaikosa, kumbuka shetani anao mawakili wake hata katikati ya kusanyiko la wana wa Mungu.
Shetani👹👺 anachokifanya ni kugeuza moyo💖wa kahaba na kuufanya kuwa na hekima na upendo wa kipepo. Hapo ndipo utakuta Mwanaume ametoa mpaka nyumba yake bila kuelewa hata alichofanyiwa . Baada ya muda utasikia sijui nililogwa na maneno mengine ya kujitia tumaini.
Ili shetani👹 aweze kuwa na nafasi ndani ya ndoa anamuwekea mwanamke moyo wa kulazimisha, hivyo anapoteza nafasi yake ya ushauri kwenye ndoa, anakuwa ni mtu wa kulazimisha mambo yaende badala ya kupembeleza. Hapo ndipo shetani alipoweza kukamata wanawake wengi kwenye ndani ya kanisa.
Hivi ni vitu halisi na utakubaliana na mimi jinsi ambavyo ndoa za wapendwa zinavyoteketa kwasababu ya maharifa ya aina hii, kama wanawake wakiweza kubaki katika hii nafasi yao ya kubembeleza hakika kutakuwa na mapinduzi ya ajabu juu ya ndoa za wapendwa, Najua shetani apendi usikie ili lakini nakuombea ili upate maharifa haya jinsi yalivyo.
Mara nyingi nimesema ndani ya kanisa🏰 ili huduma niliyopewa na Mungu iendelee ndani ya kanisa lazima mumuombee Mama ( Mke wangu ) kwanini ? Nitakaporudi nyumbani na kukuta mafaili, hakika sinta kuwa na moyo uliotulia mbele za Bwana na nitashindwa kupokea sawa sawa na vile Bwana anavyotaka na utakuta nikifundisha au kuhubiri uchovu wa ndoa na matatizo ya Nyumbani. Ni muhimu sana kutambua hilo juu ya watumishi wa Mungu. Huduma aiwezi kustawi kama ukifika nyumbani badala ya kupata faraja unakutana na mafaili ya kila aina, moyo autaweza kuyabeba hayo yote nab ado ukapokea kutoka kwa Bwana.
Mithali 21:9 Ni afadhali kukaa katika pembe ya darini, Kuliko katika nyumba pana pamoja na mwanamke mgomvi.
Mwanamke mgomvi (Mwenye mafaili) anapoteza nafasi yake ya ushauri na mwanaume atakaa mahali hapo, lazima atatafuta faraja ya moyo wake maana siku zote mwanaume anatamani kufarijiwa .
Tujifunze kutoka kwa Samsoni,
Samsoni mtu mwenye nguvu sana (Mighty Power ) na tunajua jinsi Samsoni alivyowapiga, wafilisti pamoja na kumrarua simba. Wafilisti walitafuta kujua asili ya nguvu💪💪 zake lakini walishindwa ila mtu mmoja ambaye hakuwa na jeshi wala silaha ya aina yoyote aliweza kujua asili ya nguvu zake na wafilisti wakafanikiwa kile walikuwa wanakitafuta kwa Samsoni kupitia Mwanamke aitwaje Delila . Delila alimpembeleza Samsoni ili amwambie asili ya nguvu💪💪 zake, ingawa Samsoni akusema kwa mara moja ( Mara nyingi wanaume awawezi kukaa na siri kwa muda mrefu sana lakini mwanamke anaweza kukaa na siri hata kwa miaka mitano ) Delila aliendelea kumsumbua Samsoni kwa kumpembeleza sana na mwishowe alisema kile kilichokuwa ndani ya moyo wake, hapo ndipo ukawa mwisho wake. Angalia nguvu za ushawishi alizokuwa nazo Delila mpaka Samsoni alisema “Mwanamke akamwambia, Wawezaje kusema, Nakupenda; na moyo wako haupo pamoja nami? Umenidhihaki mara hizi tatu, wala hukuniambia asili ya nguvu zako nyingi. kawa, kwa vile alivyomsumbua kwa maneno yake kila siku, na kumwudhi, roho yake ikadhikika hata kufa.”
Roho ya Samsoni ikadhikika hata kufa siyo kitu cha kawaida kwasababu ya nguvu za ushawishi ndani ya mwanamke ukisoma Mistari ya juu ya Waamuzi 16 Utakuka Delila akimwambia Samsoni Tazama, umenidhihaki, na kuniambia uongo; sasa tafadhali, niambie, waweza kufungwa kwa kitu gani?” Kuna kipindi Delila alimwambia Samsoni wawezaje kusema unanipenda na huku unanificha . Mwanamke ana nguvu ya ajabu sana lazima uelewe ili na ndiyo maana tunahitaji kurudisha asili ya mwanamke aliyoibiwa ili kuponyesha ndoa zetu 💑.
Kwanini Shetani anawanyanganya wanawake wenye haki ya Mungu wasiwe na kinywa cha kubembeleza.
Shetani anajua ili avunje ndoa anaachilia uchovu wa moyo, manung’uniko ya kutaka haki na kufanya mwanamke ashindwe kupembeleza. Kila mara mwanamke wa namna hiyo anaona ameonewa bila kutambua mamlaka yaliyepo ndani yake.
Mithali 21:19 Ni afadhali kukaa katika nchi ya nyika; Kuliko na mwanamke mgomvi, mchokozi
Mithali 18:12 Apataye mke apata kitu chema; Naye ajipatia kibali kwa Bwana.
Kwa leo tuishie hapa …..
Nawakaribisha katika semina ya wanandoa itakayofanyika 2/12/2016 Ni semina ya Nguvu tutakuwa na watumishi mbali mbali wakifundisha juu ya Ndoa. Wewe ambaye ndoa yako iko katika hali ya hatari tambua lipo tumaini njoo wewe na mwenza wako Bwana atakupa majibu ya Ndoa yako . Kwa maelezo zaidi juu ya semina na utaratibu tafadhali usisite kuwasiliana na Kanisa la Power of God kwa Adress iliyepo hapo chini.
Mungu akubariki na Siku Njema
Bishop Dankton Rudovick Rwekila
Chanika Buyuni
Dar es salaam, Tanzania
Tel: +255 753 230 680 +255 717 538 499
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment