Papa akikamilisha ziara yake Mashariki ya Kati
Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis
amezungumzia janga la mateso dhidi ya wayahudi wakati wa utawala wa
Nazi- maarufu kama Holocaust, wakati wa ziara yake katika makavazi ya
Yad Vashem Holocaust mjini Jerusalem.
Aliweka shada la maua katika ukumbi huo wa
ukumbusho na kusikiza hadithi za manusura wa janga hilo baya la
kihistoria kuwai kuwakumba wayahudi.Awali Papa alizuru eneo la kumbukumbu la wayahudi waliouwawa kutokana na mashambulio ya kigaidi pamoja na kuomba katika maeneo takatifu kwa waisraeli magharibi mwa ukuta huko Jerusalem
Papa anakamilisha ziara yake ya siku tatu mashariki ya kati hii leo kwa kuzuru msikiti wa zamani wa al-Aqsa na kuwaomba waislamu kuwa na upendo.
Amapokelewa vyema na waisraeli na wapalestina na hata kuwaalika marais wa nchi hizo katika Vatican
Viongozi hao wawili Shimon Peres wa Israel na Mahmoud Abbas wa Palestina wameelezea matumani ya kumtemblea Papa.
Akiongea na mufti wa Jerusale, Ppa alitoa wito kwa wakristo, wayahudi na waisilamu kupendana.
No comments:
Post a Comment