Hata na mgeni naye, asiyekuwa mmoja wa watu wako Israeli, atakapokuja kutoka nchi iliyo mbali sana kwa ajili ya jina lako kuu, na mkono wako ulio hodari, na mkono wako ulionyoshwa; hao watakapokuja na kuomba wakiielekea nyumba hii; 2 Wafalme 6:32.

Saturday, 16 July 2022

BETHLEHEM

 West Bank






The West Bank city of Bethlehem, about 9km south of Jerusalem, is celebrated by Christians as the birthplace of Jesus Christ.

Here Mary gave birth in a cave used for animals. Here the local shepherds came to worship the baby, and here the Three Wise Men from the east came to pay homage and present their gifts.

Here too, 1000 years before Christ, Bethlehem was the birthplace of David, Israel’s second king. Here David was anointed as king by the prophet Samuel after being brought in from tending his father’s sheep.

The city of Bethlehem (in Hebrew its name means “house of bread”) perches on a hill at the edge of the Judaean desert. Bedouin from the desert rub shoulders with pilgrims and tourists among a mix of cultures in its town market and its narrow, ancient streets.

 

Cave can be visited

The Gospel references to Christ’s birth are sparse. The physician Luke gives most information: “And so Joseph went from the town of Nazareth in Galilee to Judea, to David’s town of Bethlehem — because he was of the house and lineage of David — to register with Mary, his espoused wife, who was with child . . . . She gave birth to her first-born Son and wrapped him in swaddling clothes and laid him in a manger, because there was no room for them in the place where travellers lodged.” (Luke 2:4,7)


The cave where the birth took place and the manger stood can now be visited underneath the huge Basilica of the Nativity. This is the oldest complete church in the Christian world.

During the 20th century, Bethlehem was controlled in turn by Turkey, Britain, Jordan and Israel. Hostilities led to thousands of displaced Palestinians living in official refugee camps nearby.

In 1995 Bethlehem came under the administration of the Palestinian Authority, though Israel retained control of entrances and exits. During times of Israeli-Palestinian conflict, the city has seen many confrontations.

Israel’s construction of the separation wall has severely affected Bethlehem’s economy and the movements of its residents. The barrier runs along the city’s northern side, within metres of houses.

 

Most residents are Muslims

Because of Christian emigration, Bethlehem now has a Muslim majority. The Mosque of Omar is a prominent landmark.


The remaining Christians include Latin, Syrian, Melchite, Armenian and Maronite Catholics; Greek, Syrian and Armenian Orthodox; and a variety of Protestant denominations. Many religious institutions are present, including Bethlehem University, founded under the direction of the Vatican.

Maintaining the Christmas spirit, Franciscan friars daily celebrate the Eucharist in the Grotto of the Manger and at noon perform a procession around the holy places.

Bethlehem’s residents, who depend largely on pilgrims and tourists for their livelihood, are known for their olive wood carvings, mother-of-pearl jewellery (a craft introduced by the Franciscans) and distinctive embroidery.

In the words of one pilgrim, Della Shenton, “Bethlehemites are cheerful, peaceful, gentle people, who have welcomed pilgrims for centuries: They now stand waiting for visitors. Jesus Christ was born here, their expressions appear to say; so where are all the Christians?”

CONTACT US









KUHUSU SISI


Wednesday, 13 July 2022

HIJA (PILGRIM)

 UTANGULIZI

1 Nalifurahi waliponiambia, Na twende nyumbani kwa Bwana. Miguu yetu imesimama Ndani ya malango yako, Ee Yerusalemu. Ee Yerusalemu uliyejengwa Kama mji ulioshikamana, Huko ndiko walikopanda kabila, Kabila za Bwana; Ushuhuda kwa Israeli, Walishukuru jina la Bwana. Maana huko viliwekwa viti vya hukumu, Viti vya enzi vya mbari ya Daudi. Utakieni Yerusalemu amani; Na wafanikiwe wakupendao; Amani na ikae ndani ya kuta zako, Na kufanikiwa ndani ya majumba yako. Kwa ajili ya ndugu zangu na rafiki zangu Niseme sasa, Amani ikae nawe. Kwa ajili ya nyumba ya Bwana, Mungu wetu, Nikutafutie mema. Zaburi 122:1-9

Hija ni ziara ya kidini yaani ni safari inayofanyika kwa sababu ya dini ikilenga patakatifu fulani. Hujaji na mtalii wanaweza kufuata ratiba hiyo hiyo, lakini hujaji yuko katika safari takatifu ambayo Mungu anakutana naye kupitia mahali, watu na hali.

Mtalii huona vituko, hugundua maeneo mapya, hujifunza mambo ya kuvutia, huchukua picha na kukusanya zawadi. Mtalii anarudi nyumbani mtu sawa na yule aliyeondoka, ila labda kwa akili iliyo na mambo mengi zaidi. Hujaji hupata utambuzi na kutambua ukweli mpya kuhusu yeye mwenyewe. Hujaji husafiri kwa matarajio kuwa mwenye kurejea hatakuwa sawa na yule aliyetoka. Matokeo ya hija yatakuwa ni mabadiliko yaliyotokea ndani ya mtu. Hija atarudi na hisia iliyochapishwa kwenye nafsi, badala ya kumbukumbu ya kamera ya digitali.

Sababu ya kwenda mahali maalumu ni tumaini la kuwa karibu zaidi na imani mahali ambako mambo muhimu ya historia ya dini husika yalitokea; mara nyingi pia imani ya kwamba maombi yatakuwa na nguvu au mafanikio zaidi pale.

Desturi ya kuhiji iko katika dini mbalimbali.

·      Uyahudi tangu zamani unatia maanani hasa hija ya kwenda Yerusalemu, iliyokuwa ya lazima katika sikukuu mbalimbali kwa waumini kuanzia umri wa kubalehee; unaendelea hata baada ya hekalu la mji huo kubomolewa kabisa mwaka 70 BK.                                           

·      Wakristo hasa wa madhehebu ya Kiorthodoksi na Katoliki wanajua hija kwenda Yerusalemu, Roma na mahali pengine.

Kitabu hiki kimelenga kufanikisha hija yako katika Nchi Takatifu ya Israeli pekee kwa kukuonyesha maeneo muhimu ambayo yapo ndani ya maandiko matakatifu. Ni rahisi sanaa kupanga kwenda Israeli kwaajili ya maombi lakini usipojue eneo gani linahusika na aina ipi ya maombi unaweza kurudi bila kile ulichotarajia. 

Roho Mtakatifu amefunua siri zake kwetu ili tuweze kufanikisha hija yako na kuwa na matokeo chanya kwenye maombi yako kwa ujumla. Mara nyingi wanaotuongoza (guide) kwenye safari hizi za Nchi takatifu wanatupa historia ambayo ukichunguza kwa makini ni kitu walichosomea kwa miaka mingi, na hakina mafanikio makubwa sana kwenye maisha yako ya kiroho. 

Unaweza kujiuliza swala kwamba hii inakuwaje kusema ni historia tu?

Tuangalie kidogo kwenye maandiko Matakatifu ambayo ndiyo kiongozi wetu kama waamini wa Kristo. 

Matendo Ya Mitume 8:27-40

27 Naye akaondoka, akaenda; mara akamwona mtu wa Kushi, towashi, mwenye mamlaka chini ya Kandake malkia wa Kushi, aliyewekwa juu ya hazina yake yote; naye alikuwa amekwenda Yerusalemu kuabudu, 28 akawa akirejea, ameketi garini mwake akisoma chuo cha nabii Isaya. 29 Roho akamwambia Filipo, Sogea karibu na gari hili, ukashikamane nalo. 30 Basi Filipo akaenda mbio, akamsikia anasoma chuo cha nabii Isaya; akanena, Je! Yamekuelea haya unayosoma? 31 Akasema, Nitawezaje kuelewa, mtu asiponiongoza? Akamsihi Filipo apande na kuketi pamoja naye. 32 Na fungu la Maandiko alilokuwa akilisoma ni hili, Aliongozwa kwenda machinjoni kama kondoo, Na kama vile mwana-kondoo alivyo kimya mbele yake amkataye manyoya, Vivyo hivyo yeye naye hafunui kinywa chake. 33 Katika kujidhili kwake hukumu yake iliondolewa. Ni nani atakayeeleza kizazi chake? Kwa maana uzima wake umeondolewa katika nchi. 34 Yule towashi akamjibu Filipo, akasema, Nakuomba, nabii huyu; asema maneno haya kwa habari ya nani; ni habari zake mwenyewe au za mtu mwingine? 35 Filipo akafunua kinywa chake, naye, akianza kwa andiko lilo hilo, akamhubiri habari njema za Yesu. 36 Wakawa wakiendelea njiani, wakafika mahali penye maji; yule towashi akasema, Tazama, maji haya; ni nini kinachonizuia nisibatizwe? 37 Filipo akasema, Ukiamini kwa moyo wako wote, inawezekana. Akajibu, akanena, Naamini ya kwamba Yesu Kristo ndiye Mwana wa Mungu.] 38 Akaamuru lile gari lisimame; wakatelemka wote wawili majini, Filipo na yule towashi; naye akambatiza. 39 Kisha, walipopanda kutoka majini, Roho wa Bwana akamnyakua Filipo, yule towashi asimwone tena; basi alikwenda zake akifurahi. 40 Lakini Filipo akaonekana katika Azoto, na alipokuwa akipita akahubiri Injili katika miji yote, hata akafika Kaisaria.

Alipokuwa anaenda kuabudu kwa lugha ya kawaida alikuwa anaenda kushiriki ibada, kwa tafsiri ya kuabudu au kwa lugha ya sasa ambayo wengi tunafahamu tungesema amekwenda hija.  

Huyu mtu ameshuka kwenda Yerusalemu kutoka Kushi ambayo ni Ethiopia kwa sasa. Kutoka Ethiopia mpaka Israeli ni kama miles 1,550. Kwa vyovyote alitumia gharama kwaajili ya matayarisho ya safari yake na alijua umuhimu wa kwenda Yerusalemu kuomba. Nataka uone kwamba hizi safari za kwenda mahali kwaajili ya kuutafuta uso wa Bwana hazikuanza katika kipindi cha karne ya sasa ni miaka mingi iliyopita. 

Huyu mtu ameenda ibadani hajaokoka hajamjua Mungu, lakini ndani yake anatafuta kumjua Mungu sio kanisa. Biblia inaita kuabudu hatafuti kulijua kanisa bali kumjua huyo Mungu, alietengeneza ile madhabahu ikawepo na watu wanajikusanya wanasema wanaenda kuabudu. Madhabahu maana yake ni mahali ambapo watu wameweka mahusiano na Mungu wao na wametengeneza mahali pa kukutana nae huyo Mungu wao. Sasa huyu ndugu ametoka kwenye ibada hajaona alichokuwa anatafuta, kwa sababu hajaenda kusali tu kama kusali, alienda kutafuta mahusiano yake na Mungu. Na Biblia inasema yeyote amtafutaye kwa bidii atamuona haijalishi ni wa kabila na dini gani ndani yake kama ana kiu Mungu hataficha uso wake kuna namna ambavyo atajifunua kwake.

Nataka kukueleza juu ya umuhimu wa kufanya hija yenye nguvu za Mungu si swala la kusafiri na kwenda Nchi takatifu tu. Maandiko yanasema wazi kwamba “Watu hawa huniheshimu kwa midomo; Ila mioyo yao iko mbali nami. Nao waniabudu bure, Wakifundisha mafundisho Yaliyo maagizo ya wanadamuMathayo 15:8-9. Nataka uone lile neno linasema nao waniabudu bure”unaweza kwenda Israeli na ikawa bure pasipokuwa na muongozo sahihi wa kitu gani chakufanya. Madhumuni makubwa ya kitabu hiki ni kuhakikisha kwamba unakwenda na kupata kila ambacho Mungu amekusudia kwa kila mmoja anayekwenda na kuutafuta uso wake. 

Nimeona watu wengi sana wakipinga swala hili la kwenda Israeli na wengine wakisema hakuna umuhimu kabisa na wananukuu maandiko kabisa. Unajua katika hali ya Imani ni muhimu kuwa makini kwamba unamsikia nani na anaongozwa na nani? Siyo kila jambo watu wote wanafunuliwa na ndiyo maana Siri ya Bwana iko kwao wamchao, Naye atawajulisha agano lake.Zaburi 25:14.Kinachokuza Imani yako ni namna unavyolicha jina la Bwana na namna unavyotetemeka mbele zake na kumuelewa yeye kupitia neno lake si kwenda Israeli pekee. Jaribu kufikiri safari ya siku tano kila siku tunaongelea Biblia tu pekee bila kuchanganya na mambo mengine mengi simu za nyumbani na mambo ya kazini kwako lazima kuna neno litaingia ndani yako. Nasi tunatenga siku hizi za hija maalumu kwaajili ya kuomba na kutafakari ukuu wa Mungu tukiwa maeneo ambayo Biblia iliandikwa huko. 

Huyu ndugu alikwenda Hekaluni akiwa na kiu ya kumuona Mungu aliyeziumba mbingu na Nchi na akiamini kabisa kama vile kitabu cha 2 Nyakati 7:14kinavyosema “ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekesha, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao.Kwa hivyo alikuwa na uwakika wa kusema na Mungu lakini maandiko yanasema alikuwa anarudi kwao Ethiopia bila kujua kitu au kupata kile alitarajia kupata kweye ibada yake. 

Ni rahisi sana kusoma habari za huyu ndugu na usijue kile kiliendelea na kiu iliyokuwa ndani yake hata kupelekea Filipo aliyekuwa kwenye uamsho mkubwa wa injili huko Samaria kuambiwa aende kwa huyu ndugu. Sasa kile kilichovuta nguvu za Mungu ni aina ya kiu aliyekuwa nayo huyu ndugu ndipo Bwana akajibu na kumtuma Filipo. 

Bwana ametupa nafasi hii ili kuweka kiu ndani yako ili kabla haujafika Nchi takatifu ujue ni namna gani ya kuomba katika maeneo tofauti tofauti. Kila eneo linakusudi lake na yapo mambo mengi sana yametendeka kwa kila eneo. 

Israeli ni Nchi ambayo imejaa vitu vingi sana ambavyo kiuhalisia kila kimoja ni cha kiimani inategemeana na namna unavyoona maandiko yanasema “Maana aonavyo nafsini mwake, ndivyo alivyo. Akuambia, Haya, kula, kunywa; Lakini moyo wake hauwi pamoja nawe” Mithali 23:7. Namna unavyoona kila kitu ndivyo itakavyokuwa kwako ukiona umekwenda kwa misingi ya utalii utapata hicho hicho. Lakini ukienda kwaajili ya hija hakika utapata vile unavyotaka katika hija yako. Tumeweka kitabu hiki kwenye mikono yako kwa kusudi la kukuongoza kwa kila eneo la hija yako ili ufurahie na kupata matokeo mazuri kwenye maisha yako hapa Duniani. 

Kuna mambo ya kihistoria ambayo kimsingi utayapata sana ukiwa Nchini Israeli lakini kwenye kitabu hiki nikuhakikishie tu kwamba tutakutazamisha yale ambayo ni ya Rohoni kwaajili ya msaada wa hija yako. Kumbuka jambo hili kila mara hija ni safari ya kiroho kwaajili ya mahali fulani Patakatifu. Najua kabisa watu wengi wamekwenda katika Nchi takatifu na wengine wamerudi wakiwa na tumaini jipya na wengine wamerudi katika hali ya kawaida kabisa ni matumaini yangu kwamba safari yako haitakuwa yakawaida katika maisha yako. Tumekuandalia kitabu hiki ili kikuwezeshe na kukuongoza katika hija yako na kukupa mwanga wa kiroho. Kitabu hiki kimejaa mambo ambayo mengi sana utakutana nayo maeneo husika lakini ni kiongozi kwaajili ya maswali yako ambayo unaweza kuwa nayo katika kipindi chote cha safari yako. 

Safari hizi ni ibada katika maisha yako, na tunatumaini katika utumishi huu utafurahia na kusonga mbele kwenye maisha yako. 

Kitabu hiki tumekigawa katika sehemu kuu mbili sehemu ya kwanza inahusiana na historia ya kawaida ya maeneo muhimu ya Israeli, na maeneo mengine kama Misri na Yordani sehemu ya pili inahusiana na muongozo wa kimaombi wa kila eneo ambalo ni la kihistoria kulingana na maandiko matakatifu. 

Katika Safari yako ni muhimu kwenda na kanuni hizi:

      I.        Kabla ya hapo, tarajia kile utakachoona kwa kusoma kukihusu.

    II.        Unapofika hapo, karibia eneo kwa matarajio yote unayoweza kupata, kana             kwamba ni sehemu pekee duniani ambayo ni muhimu.

  III.        Unapofika, tambua uwepo wake Mtakatifu, ukichukua muda kuwa peke yako, wewe mwenyewe na Mungu.

 IV.        Baada ya kuondoka, andika mawazo yako ya baadae kuhusu yale uliyopitia.

Karibu kwenye safari yenye nguvu za Mungu kwenye maisha yako. 

Mungu akubariki sana. 

Pastor Daniel Lema. 

Wednesday, 9 November 2016

🔪🔪🔪*KUMKATA MWASHURU VIPANDE VIPANDE*



Na Bishop Dankton Rudovick Rwekila


Mungu anataka kukufungua ili uweze kuwa na uhuru wako wa kuchagua jambo jema au baya . Uzima na mauti . Kuna watu awapendi Sigara,🚬 Pombe🍺 na vitu vya aina hiyo au vile vitu visivyompendeza Mungu🚫.


Isaya 14:24-25 Bwana wa majeshi ameapa, akisema, Hakika yangu kama vile vilivyoazimia, ndivyo itakavyokuwa; na kama nilivyokusudia, ndivyo itakavyotokea;  kwamba nitamvunja huyo Mwashuri vipande vipande katika nchi yangu, na juu ya mlima wangu nitamkanyaga chini ya miguu yangu; ndipo nira yake iliyo juu yao itakapoondoka, na mzigo wake utatoka mabegani mwao.

Isaya 43:1-2 Lakini sasa, Bwana aliyekuhuluku, Ee Yakobo, yeye aliyekuumba, Ee Israeli, asema hivi, Usiogope, maana nimekukomboa; nimekuita kwa jina lako, wewe u wangu. Upitapo katika maji mengi nitakuwa pamoja nawe; na katika mito, haitakugharikisha; uendapo katika moto, hutateketea; wala mwali wa moto hautakuunguza.


Shetani👹 amekufunga🔗🔗 ili ukae kwenye maamuzi ambayo siyo ya kwako.📖Biblia inasema nimeweka uzima na mauti mbele yako , chagua uzima ili uwe ili uwe hai, wewe na uzao wako (Kum 30:19)


Wakati Roho Mtakatifu ananifundisha juu ya somo hili alinichukua mpaka kwenye mfano wa gari🚘 ambalo limejaa mafuta⛽ na Dereva👷 ambaye amepanga safari na kuhakiki kwamba mafuta yatamfikisha katika safari yake anayokwenda, yawezekana mafuta aliyoweka yanamfikisha Morogoro lakini kufika ubungo, mafuta⛽ yameisha kwa maana nyingine tank limetoboka 🚘.


👩‍👩‍👧‍👧Ndivyo inavyotokea kwa Mkristo ambaye ametoka kanisani🏰 na amempokea Roho Mtakatifu na kujazwa Nguvu za Roho Mtakatifu, lakini unapofika njiani unarudi katika hali yako ya kawaida ya dhambi kabla aujafika kule ambako Roho Mtakatifu alitaka ufike, kwenye kazi yako , Biashara yako , Kampuni yako , Ndoa yako n.k


Kupokea Roho Mtakatifu ni jambo moja, kuishi naye ni jambo jingine, na kukubali akuongoze ni jambo lingine.


Unapokea Nguvu💪 kwasababu ya kazi yako na wakati unaelekea kwenye kazi yako ghafla mambo ya Dunia 🌏yanaanza kukusonga na unajikuta ukitenda dhambi ambayo ni machukizo mbele za Mungu maana yake safari inaishia hapo na unakwama kabisa japo ulipokea nguvu ya kutosha kabisa.


Ndiyo maana kwenye maombi unasikia nguvu💪 ya Mungu  kububujika lakini tukiangalia maisha yako halisi hakuna hatua 🚶ambayo umepiga kwenye maisha yako ya wokovu.


JE MUNGU ANAONGOZA MAISHA YAKO ?
Matendo 4:29  Basi sasa, Bwana, yaangalie matisho yao; ukawajalie watumwa wako kunena neno lako kwa ujasiri wote, ukinyosha mkono wako kuponya; ishara na maajabu vifanyike kwa jina la Mtumishi wako mtakatifu Yesu. Hata walipokwisha kumwomba Mungu, mahali pale walipokusanyika pakatikiswa, wote wakajaa Roho Mtakatifu, wakanena neno la Mungu kwa ujasiri. Na jamii ya watu walioamini walikuwa na moyo mmoja na roho moja; wala hapana mmoja aliyesema ya kuwa kitu cho chote alicho nacho ni mali yake mwenyewe; bali walikuwa na vitu vyote shirika.  Na mitume wakatoa ushuhuda wa kufufuka kwake Yesu kwa nguvu nyingi, na neema nyingi ikawa juu yao wote.  Wala hapakuwa na mtu mmoja miongoni mwao mwenye mahitaji; kwa sababu watu wote waliokuwa na viwanja au nyumba waliviuza, wakaileta thamani ya vitu vile vilivyouzwa,


Walipokea Nguvu💪 na walikuwa na nia moja, ni muhimu kuangalia maisha yako je wewe una nia moja katika Kristo Yesu, kwasababu ukiangalia kanisa🏰 la sasa kila mtu anajiangalia mwenyewe na kujiongoza kwa namna inavyompasa yeye mwenyewe, Chuki zimejaa ndani ya kanisa🏰 na manunguniko kila siku yanazidi kutafuna kanisa la Bwana.


Wengi katika kanisa leo wamebaki wakihesabu ni miaka mingapi sasa wameokoka, bila kuangalia maendeleo yao katika wokovu.

 Unafanya dhambi leo kisha kesho unatubu siku mbili mbele kabla hata ya muujiza wako unaanguka tena kwenye dhambi, miaka nenda rudi.

Ni sawa na mtoto wa Rais wa Nchi fulani au mtoto wa tajiri mwenye fedha 💰💸💸💵💴nyingi na madaraka makubwa, lakini mtoto wake analia njaa na kulala nje kila siku huku akijisifu Baba yake ni Rais au tajiri. . Mungu wetu ndiyo mwenye vyote na sisi kama watoto wake ni warithi sawa sawa na ahadi zake lakini maisha tunayoishi ni ya watoto wasio na BABA.


MTU MWENYE ROHO MTAKATIFU ANAKUWA NA MAMBO SABA AMBAYO YANAASHIRIA KUWA ANAONGOZWA NA ROHO


1⃣ Nguvu ya Upendo
2⃣Nguvu ya kushirikiana katika moyo mmoja

3⃣Nguvu ya kuambatana bila Kukata tamaa kwa moyo mmoja

4⃣Nguvu ya kuhurumiana inayotoka katika moyo wa kweli (Huruma ya KIUNGU) Katika huruma ni muhimu kupima huruma ya shetani na MUNGU. Huruma ya shetani inaambatana na sifa za kujitukuza mwenyewe, Huruma ya KIUNGU inamtukuza Mungu peke yake.

5⃣Nguvu ya kusamehe . Aijalishi aina ya kosa Biblia inasema Jua lisichwe na uchungu wenu bado haujawatoka. Waefeso 4:26

6⃣Nguvu ya kuomba msamaha. Aliye na Roho Mtakatifu ni mwepesi wa kuomba msamaha

7⃣Nguvu ya kumuheshimu MUNGU na watumishi wake.



Unapokuwa na mambo hayo tanki lako linakuwa salama na alijatoboka, Ili hatua saba hizi zitokee kwako ni lazima upitie hatua tatu muhimu

1⃣Kumpokea Roho mtakatifu.

2⃣Kuishi naye.

3⃣Kuongozwa na Roho Mtakatifu.



Mungu akubariki sana,


Bishop Dankton Rudovick Rwekila
Chanika Buyuni
Dar es salaam, Tanzania
Tel: +255 753 230 680 +255 717 538 499

👩*KURUDISHA NAFASI YA MWANAMKE ILIYOPOTEA NDANI YA KANISA , FAMILIA NA TAIFA*👩



Na Bishop Dankton Rudovick Rwekila


Wakati tunarudisha nafasi ya mwanamke👩 kwenye familia👪, kanisa, taifa na Dunia🌍 kwa ujumla , ni muhimu kuweza kutambua ni nafasi ipi iliyopotea.


MOYO💖 WA USHAURI ULIOAMBATANA NA HEKIMA YA USHAURI

Mungu alimuumbia mwanamke Roho ya uvumilivu, Mwanamke akiliamini jambo na kulipenda anasimamia kwa nguvu zake zote. Mwanaume akipenda jambo anakuwa anachunguza chunguza. Ndiyo maana hata katika hali ya kanisa🏰 katika kububujika na kumpokea Roho Mtakatifu ni wanawake ndiyo wa kwanza , Hata wakati wa Bwana Yesu kwenda kumuona kaburini ( Mathayo 28:1)


Hawa👩 alikuwepo kwaajili ya ushauri kwa Adamu👷. Mwanamke aliporidhika na maelezo ya Nyoka🐍 moyo wake ukabadilika na akalipeleka kwa Mume wake


Shetani hali akijua nguvu iliyopo ndani ya mwanamke ya ushawishi ndiyo maana misuko suko mingi sana inawakuta wanawake. Shetani anajua nguvu ya ushawishi wa mwanamke, ndani ya familia👪 ndiyo maana anaweka uchungu mkubwa ndani ya moyo💖 wake na kutoa moyo wa ushauri ambao ndiyo asili lake.

 Moyo wenye uchungu wa mwanamke utashauri, uchungu, mawazo yake binafsi, uchovu. 📖Biblia inasema kiujazacho 💖Moyo ndicho kimtokacho mtu ndicho kimeujaza moyo wake.


Mwanamke anaweze kusema jambo leo na wakati mwingine kwasababu ya 👷ubaba , Mwanamume anafanya kwa kuamrisha ila Mwanamke atahakikisha kile ambacho amekitaka kinakuwa vile vile hata baada ya miaka mitano👊, atatumia nguvu yake ya ushawishi na utakuta mwanaume akikubaliana naye baada ya Muda mfupi. Mara nyingi mwanaume jambo lake ni papo kwa papo. Mwanaume usahau mapema ila ni tofauti kwa mwanamke atalifanyia kazi jambo mpaka litimie.


Kwenye familia Mama akikupenda💝 hata Baba asipokupenda tambua kwamba ipo siku kutokana na ushawishi wa mama, Baba atakupenda tu kutokana na nguvu iliyopo ndani ya mwanamke , inayoambatana na moyo wa ushawishi. Mwanamke amepewa nafasi ya kubadili familia.👪


Mwanamke kwa nafasi aliyopewa ya Moyo wa ushauri unaweza kufungua baraka ndani ya Nyumba 🏡



📖_2 Wafalme 4:9-16 Yule mwanamke akamwambia mumewe, Tazama, mimi naona ya kuwa mtu huyu apitaye kwetu mara kwa mara ni mtu mtakatifu wa Mungu. Nakuomba, tumfanyie chumba kidogo ukutani; na ndani yake tumwekee kitanda, na meza, na kiti, na kinara cha taa; na itakuwa, atujiapo, ataingia humo. Ikawa siku moja akafika huko, akaingia katika chumba kile akalala. Akamwambia Gehazi mtumishi wake, Mwite yule Mshunami. Naye alipokwisha kuitwa, akasimama mbele yake.  Akamwambia, Sema naye sasa, Tazama, wewe umetutunza sana namna hii; utendewe nini basi? Je! Uombewe neno kwa mfalme, au kwa amiri wa jeshi? Yule mwanamke akamjibu, Mimi ninakaa katika watu wangu mwenyewe.  Akasema, Basi, atendewe nini? Gehazi akajibu, Hakika hana mwana, na mumewe ni mzee.  Akamwambia, Kamwite. Naye alipokwisha kuitwa, akasimama mlangoni. Akasema, Panapo wakati huu mwakani, utamkumbatia mwana. Akasema, La! Bwana wangu, wewe mtu wa Mungu, usiniambie mimi mjakazi wako uongo.


Mwanamke huyu tunayemsoma📖 katika habari hii anamshauri mumewe kujenga chumba🏡 kwaajili ya watumishi wa Mungu ambao hata mume wake alikuwa awajui. Lakini kwasababu ya ushawishi na nguvu ya ushauri ya mwanamke malango ya Baraka yalifunguliwa ndani ya nyumba yao.


Mwanamke akimkaribisha mtu nyumbani mwake mwanaume awezi kukataa, lakini sivyo kwa kwa mwanaume , unaweza kutumia ubavu💪 lakini, kutokana na nguvu ya ushawishi na ushauri wa mwanamke mtu huyo ataondoka tu.


✔Mwanamke si mtawala lakini anayo mamlaka tena yenye nguvu. Ni sawa sawa na Rais, Bunge na Mahakama kila muhimili unamamlaka yake tena yenye nguvu. Ndiyo maana Biblia📖 inasema mwanamke mpumbavu uivunja nyumba yake kwa mikono yake mwenyewe.

Mfano wa Esta

Esta 5:1-8

Ikawa siku ya tatu Esta alijivika mavazi yake ya kifalme, akasimama katika ua wa ndani wa nyumba ya mfalme, kuielekea nyumba ya mfalme; naye mfalme akaketi juu ya kiti chake cha enzi katika nyumba ya mfalme, kuuelekea mlango wa nyumba. Ikawa, mfalme alipomwona malkia Esta amesimama uani, yeye akapata kibali machoni pake; naye mfalme akamnyoshea Esta fimbo ya dhahabu aliyokuwa nayo mkononi. Basi Esta akakaribia, akaigusa ncha ya fimbo.Mfalme akamwambia, Malkia Esta, wataka nini? Nayo ni haja gani uliyo nayo? Utapewa hata nusu ya ufalme.  Esta akasema, Mfalme akiona vema, na aje leo, mfalme na Hamani, kwenye karamu niliyomwandalia. Basi mfalme akasema, Mhimize Hamani, ili ifanyike kama Esta alivyosema. Hivyo mfalme na Hamani wakafika katika karamu ile aliyoiandaa Esta.
 Basi mfalme akamwambia Esta pale penye karamu ya divai, Dua yako ni nini? Nawe utapewa; na haja yako ni nini? Hata nusu ya ufalme utafanyiziwa. Esta akajibu, na kusema, Dua yangu ni hii, na haja yangu ni hii, Ikiwa nimepata kibali machoni pa mfalme, na mfalme akiona vema kunipa niombalo, na kunifanyizia haja yangu, na aje tena mfalme na Hamani kwenye karamu nitakayowaandalia, nami kesho nitafanya kama vile mfalme alivyosema.

Unaposoma Mistari ya hapo ☝juu na ukiangalia yale ambayo Esta alitaka kumuambia Mfalme utagundua Esta alikuwa na Siri nzito sana ndani ya Moyo💖 wake. Hata wakati anamkaribisha mume wake kwenye chakula🍝 na kwasababu ya nguvu ya ushawishi alimshawishi aje na Hamani .

Jambo kubwa ambalo lazima uone kwa macho tofauti ni pale mfalme alipomwambia Esta hata nusu ya ufalme💔 wake atampa, lakini Esta alikuwa na jambo lake ambalo aliitaji bado kulipika ndani ya moyo wa Mfalme . Unapoendelea na Mlango ule wa Saba utaona ombi la Malkia Esta . Kumbuka jambo moja Esta hakuwa mke pekee wa mfalme , Mfalme alikuwa na wake wengi na unaweza kufikiri kama angetoa nusu ya ufalme wake kwa Esta ambaye hakuwa na tamaa ya ufalme hao wengine wangekuwa katika hali gani.

Kupitia huu mfano wa Esta nataka nikuambie Siri ambayo makahaba wengi wanatumia kwaajili ya kuteka ndoa nyingi za wakristo. Mwanaume anarudi nyumbani akiwa mchovu na shughuli z hapa na pale, anamkuta mke Nyumbani badala ya kupokelewa na tabasamu anapokelewa na maneno ( Mimi nayaita mafaili) Mke anafungua faili la kila aina badala ya faraja na kubembelezwa huyu mwanaume tena aliyeokoka, anapokelewa kwa staili hiyo, Na Mwanaume wakati huo unahitaji kupembelezwa ili kesho unapoamka anakuwa na nguvu mpya kwasababu yupo mshauri ambaye amesimama katika nafasi yake. Anaitaji maneno matamu kama “Pole kwa kazi mume wangu, najua umechoka na kazi na najua pia changamoto za kazi/ Huduma ni nyingi sana lakini usijali mimi niko upande wako aijalishi hata kama unasemwa vibaya mimi niko upande wako, hata kama aujapata leo najua kesho utapata mume wangu, Mungu yupo upande wetu usiofu kabisa“ Sasa haya ni maneno baadhi tu yapo mengi mno ambayo hakika yanapotumika mtu usahahu kabisa kama alikuwa na changamoto za hapa na pale kwenye huduma au kwenye jambo lolote analolifanya kwa kusudi la Mungu. Lakini mtu huyu akafika nyumbani na kukutana na mafaili na anapokelewa nayo alafau kesho yake akutane na mtu anayejua kubembeleza hakika hii ndoa ya Kikristo tunaikosa, kumbuka shetani anao mawakili wake hata katikati ya kusanyiko la wana wa Mungu.

Shetani👹👺 anachokifanya ni kugeuza moyo💖wa kahaba na kuufanya kuwa na hekima na upendo wa kipepo. Hapo ndipo utakuta Mwanaume ametoa mpaka nyumba yake bila kuelewa hata alichofanyiwa . Baada ya muda utasikia sijui nililogwa na maneno mengine ya kujitia tumaini.

Ili shetani👹 aweze kuwa na nafasi ndani ya ndoa anamuwekea mwanamke moyo wa kulazimisha, hivyo anapoteza nafasi yake ya ushauri kwenye ndoa, anakuwa ni mtu wa kulazimisha mambo yaende badala ya kupembeleza. Hapo ndipo shetani alipoweza kukamata wanawake wengi kwenye ndani ya kanisa.

Hivi ni vitu halisi na utakubaliana na mimi jinsi ambavyo ndoa za wapendwa zinavyoteketa kwasababu ya maharifa ya aina hii, kama wanawake wakiweza kubaki katika hii nafasi yao ya kubembeleza hakika kutakuwa na mapinduzi ya ajabu juu ya ndoa za wapendwa, Najua shetani apendi usikie ili lakini nakuombea ili upate maharifa haya jinsi yalivyo.

Mara nyingi nimesema ndani ya kanisa🏰 ili huduma niliyopewa na Mungu iendelee ndani ya kanisa lazima mumuombee Mama ( Mke wangu ) kwanini ? Nitakaporudi nyumbani na kukuta mafaili, hakika sinta kuwa na moyo uliotulia mbele za Bwana na nitashindwa kupokea sawa sawa na vile Bwana anavyotaka na utakuta nikifundisha au kuhubiri uchovu wa ndoa na matatizo ya Nyumbani. Ni muhimu sana kutambua hilo juu ya watumishi wa Mungu. Huduma aiwezi kustawi kama ukifika nyumbani badala ya kupata faraja unakutana na mafaili ya kila aina, moyo autaweza kuyabeba hayo yote nab ado ukapokea kutoka kwa Bwana.

Mithali 21:9 Ni afadhali kukaa katika pembe ya darini, Kuliko katika nyumba pana pamoja na mwanamke mgomvi.

Mwanamke mgomvi (Mwenye mafaili) anapoteza nafasi yake ya ushauri na mwanaume atakaa mahali hapo, lazima atatafuta faraja ya moyo wake maana siku zote mwanaume anatamani kufarijiwa .

Tujifunze kutoka kwa Samsoni,

Samsoni mtu mwenye nguvu sana (Mighty Power ) na tunajua jinsi Samsoni alivyowapiga, wafilisti pamoja na kumrarua simba. Wafilisti walitafuta kujua asili ya nguvu💪💪 zake lakini walishindwa ila mtu mmoja ambaye hakuwa na jeshi wala silaha ya aina yoyote aliweza kujua asili ya nguvu zake na wafilisti wakafanikiwa kile walikuwa wanakitafuta kwa Samsoni kupitia Mwanamke aitwaje Delila . Delila alimpembeleza Samsoni ili amwambie asili ya nguvu💪💪 zake, ingawa Samsoni akusema kwa mara moja ( Mara nyingi wanaume awawezi kukaa na siri kwa muda mrefu sana lakini mwanamke anaweza kukaa na siri hata kwa miaka mitano ) Delila aliendelea kumsumbua Samsoni kwa kumpembeleza sana na mwishowe alisema kile kilichokuwa ndani ya moyo wake, hapo ndipo ukawa mwisho wake. Angalia nguvu za ushawishi alizokuwa nazo Delila mpaka Samsoni alisema “Mwanamke akamwambia, Wawezaje kusema, Nakupenda; na moyo wako haupo pamoja nami? Umenidhihaki mara hizi tatu, wala hukuniambia asili ya nguvu zako nyingi. kawa, kwa vile alivyomsumbua kwa maneno yake kila siku, na kumwudhi, roho yake ikadhikika hata kufa.”

Roho ya Samsoni ikadhikika hata kufa siyo kitu cha kawaida kwasababu ya nguvu za ushawishi ndani ya mwanamke ukisoma Mistari ya juu ya Waamuzi 16 Utakuka Delila akimwambia Samsoni Tazama, umenidhihaki, na kuniambia uongo; sasa tafadhali, niambie, waweza kufungwa kwa kitu gani?” Kuna kipindi Delila alimwambia Samsoni wawezaje kusema unanipenda na huku unanificha . Mwanamke ana nguvu ya ajabu sana lazima uelewe ili na ndiyo maana tunahitaji kurudisha asili ya mwanamke aliyoibiwa ili kuponyesha ndoa zetu 💑.

Kwanini Shetani anawanyanganya wanawake wenye haki ya Mungu wasiwe na kinywa cha kubembeleza.

Shetani anajua ili avunje ndoa anaachilia uchovu wa moyo, manung’uniko ya kutaka haki na kufanya mwanamke ashindwe kupembeleza. Kila mara mwanamke wa namna hiyo anaona ameonewa bila kutambua mamlaka yaliyepo ndani yake.

Mithali 21:19 Ni afadhali kukaa katika nchi ya nyika; Kuliko na mwanamke mgomvi, mchokozi

Mithali 18:12 Apataye mke apata kitu chema; Naye ajipatia kibali kwa Bwana.

Kwa leo tuishie hapa …..

Nawakaribisha katika semina ya wanandoa itakayofanyika 2/12/2016 Ni semina ya Nguvu tutakuwa na watumishi mbali mbali wakifundisha juu ya Ndoa. Wewe ambaye ndoa yako iko katika hali ya hatari tambua lipo tumaini njoo wewe na mwenza wako Bwana atakupa majibu ya Ndoa yako . Kwa maelezo zaidi juu ya semina na utaratibu tafadhali usisite kuwasiliana na Kanisa la Power of God kwa Adress iliyepo hapo chini.

Mungu akubariki na Siku Njema


Bishop Dankton Rudovick Rwekila
Chanika Buyuni
Dar es salaam, Tanzania
Tel: +255 753 230 680 +255 717 538 499

Monday, 30 March 2015

PERFECT: Taharuki yakumba Nigeria kabla ya matokeo

PERFECT: Taharuki yakumba Nigeria kabla ya matokeo: Matokeo ya uchaguzi Nigeria yatarajiwa leo Uingereza na Marekani zimeelezea masikitiko yao kuwa kumekuwa na wizi wa kura, katika uchaguzi ...

PERFECT: Taharuki yakumba Nigeria kabla ya matokeo

PERFECT: Taharuki yakumba Nigeria kabla ya matokeo: Matokeo ya uchaguzi Nigeria yatarajiwa leo Uingereza na Marekani zimeelezea masikitiko yao kuwa kumekuwa na wizi wa kura, katika uchaguzi ...

Jopo laundwa kuchunguza viongozi Kenya

Jopo maalum limeundwa ilikuwachunguza maafisa wakuu serikalini na wanasiasa ambao wametuhumiwa kuhusika na ufisadi.

Jopo maalum limeundwa ilikuwachunguza maafisa wakuu serikalini na wanasiasa ambao wametuhumiwa kuhusika na ufusadi.
Idara ya kuchunguza masuala ya jinai,tume ya kukabiliana na ufisadi pamoja na afisi ya mashtaka ya umma zinasema zimekamilisha baadhi ya kesi.
Mashirika ya kiraia yamekua yakimshinikiza rais Uhuru Kenyatta kuwataja wote wanaotuhimiwa na ufisadi ambao umesababishia nchi kupoteza mamilioni ya pesa.
Waziri wa kilimo wa Kenya akiandamana na mawakili kadhaa, aliwasilia katika makao makuu ya tume ya kupambana na ufisadi,
muda mfupi baada ya saa sita za mchana majira ya Afrika Mashariki, huku akiwa kwenye msafara wa magari matatu ya kifahari.

Akiwa amevalia suti ya kijivu, waziri huyo alionekana mchangamfu kinyume na unavyomtarajia kiongozi aliyesimamisha kazi.

Tume ya kupambana na ufisadi ya Kenya ina siku 60 kukamilisha uchunguzi

Kabla ya kuingia ndani aliwafahamisha waandishi wa habari kuwa hana lolote hadi atakapomaliza.
Dakika arubaini na tano baadaye, Kosgei alijitokeza tena na kusema kuwa ameshauriana na mmoja wa wakurugenzi wa tume hiyo, na kinyume na alivyotarajia,
alifahamishwa kuwa kwa sasa tume hiyo haina nyaraka zozote za kuonyesha sababu zilizopelekea jina lake kuorodheshwa miongoni mwa washukiwa wa ufisadi. Kupitia kwa mawakili wake Kosgei alikuwa ametaka tume hiyo kumweleza madai dhidi yake,
orodha ya walalamishi, nyaraka zilizowasilishwa mbele ya tume hiyo na walalamishi au stakabadhi zozote kuhusiana na madai yanayomkabili.

Waziri huyo aliyesimamisha kazi itabidi asuburi hadi siku ya alhamisi wiki hii.

Punda waliwekwa katikati mwa jiji la Nairobi kuwakejeli viongozi Kenya

Mawaziri watano na maafisa wengine wengi wa taasisi za umma wamesimamishwa kazi kwa muda kuhusiana na madai ya kuhusika na ufisadi.
Akilihutubia bunge la Kenya wiki iliyopita, rais Uhuru Kenyatta aliagiza maafisa wote wakuu serikalini waliotajwa na tume ya kupambana na ufisadi
kungatuka madarakani kwa muda wa siku sitini ili kuruhusu uchunguzi wa kina.
Kwingineko, jopo maalum limeundwa ili kuchunguza madai dhidi ya mawaziri hao na maafisa wakuu serikaini,

ambo wamesimamishwa kazi nchini Kenya kuambatana na agizo la rais Kenyatta, kuwa maafisa hao wana siku sitini kukamilisha uchunguzi huo.

Punda waliwekwa katikati mwa jiji la Nairobi kuwakejeli viongozi Kenya

Jopo hilo litajumuisha maafisa kutoka idara ya mashtaka ya umma, tume ya kupambana na ufisadi na idara ya ujasusi.
Wakati huo huo maafisa wa kaunti ya nairobi leo walinasa punda watano waliokuwa wamefungwa na minyororo kati kati mwa mji mkuu.
Punda hao walikuwa wamepakwa rangi nyekundu na maandishi yanayopinga ufisadi.
Punda mmoja alikuwa na maandishi ya kimombo ''Corruption bleeding Kenya dry'' yaani Ufisadi unamaliza taifa la Kenya

Punda mwingine naye alikuwa na maandishi mengine mgongoni inayowakejeli baadhi ya wabunge wa Kenya ambao wametuhumiwa kuhusika na unyanyazaji wa kimapenzi.

Taharuki yakumba Nigeria kabla ya matokeo

Matokeo ya uchaguzi Nigeria yatarajiwa leo

Uingereza na Marekani zimeelezea masikitiko yao kuwa kumekuwa na wizi wa kura, katika uchaguzi mkuu uliomalizika siku ya Jumamosi Nchini Nigeria.
Mwaandishi wa habari wa BBC wa maswala ya Afrika aliyeko Nigeria anasema kuwa hali ni ya wasiwasi katika mji mkuu Abuja.
Katika taarifa ya pamoja, yanasema kuwa wameona dalili za kutiliwa shaka kuwa kumekuwa na uingiliaji wa kisiasa na utaratibu mzima wa uchaguzi mkuu kuvurugwa.
Aidha wachunguzi wa mataifa mengi waliokuwa wakichunguza shughuli za upigaji kura hapo siku ya Jumamosi, wamesifia uchaguzi huo.
Tume ya uchaguzi mkuu Nchini humo inasema kuwa kuna uwezekano kuwa mshindi wa uchaguzi huyo atajulikana hatimaye leo Jumatatu, na mshindi kutangazwa kesho Jumanne.

Kinyang'anyiro kikuu ni kati ya Rais wa sasa Goodluuck Jonathan na aliyekuwa kiongozi wa kijeshi Mohamadu Buhari.

Mawakala wa wagombea viti wakipiga msasa matokeo mjini Lagos

Ni ushindani mkali zaidi tangu kumalizika kwa utawala wa kijeshi miaka 16 iliyopita.
Mkuu wa Tume Huru ya Uchaguzi nchini Nigeria amesema anatumaini kumtangaza mshindi wa uchaguzi wa rais nchini humo ifikapo Jumatatu jioni.
Upigaji kura uliendelea katika siku ya pili ya uchgaguzi baada ya kutokea hitilafu katika kadi za kielektroniki na kuchelewesha usajili wa baadhi ya wapiga kura.
Kauli hiyo imetolewa na mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi, INEC, Attahiru Jega.
"Tumaini letu na ambalo tumekuwa tukilifanyia kazi kwa bidii ni kuweza kutangaza matokeo ya uchaguzi ndani ya saa arobaini na nane na tunatumaini muda mchache zaidi kuliko ule wa mwaka 2011.
Imeanza kutoka saa 48 baada ya uchaguzi kumalizika jana.
Kwa hiyo tumeanza kuhesabu saa arobaini na nane kwa kweli kutoka jana jioni wakati idadi ya kutosha ya majimbo yalipofanya uchaguzi."

Bwana Jega amesema alitumaini jumuia ya kimataifa inaweza kupongeza namna Nigeria ilivyoendesha uchaguzi.

Wasimamizi wa uchaguzi nchini Nigeria wakihesabu kura

"Tunaamini tumefanya vizuri kabisa.
Hatuwezi kupuuza changamoto tulizokumbana nazo.
Ni hakika haukuwa kamilifu lakini tunaamini kwa ujumla tumefanya vizuri sana, japokuwa bado tunayo nafasi ya kuzidi kuuboresha.
Na kwa namna yoyote ndiyo maana tuliwaalika waangalizi vikiwemo vyombo vya habari na waangalizi wengine wa uchaguzi,

ili kuweza kutangaza habari na tunaweza kujifunza kutokana na ripoti hizi na tunaweza kuendelea kuboresha mchakato wa uchaguzi.", amesema Jega.

Mama akipiga kura nchini Nigeria

Wachambuzi wa mambo wanasema ushindani ni mkubwa sana kiasi cha kushindwa kutamka mshindi ni nani.
Ujumbe wa waangalizi kutoka Umoja wa Afrika umesema uchaguzi ulikuwa wa amani lakini wamewataka wananchi wa Nigeria kukubali matokeo.
Uchaguzi nchini Nigeria umefanyika Jumamosi na Jumapili, ambapo wagombea wawili wa kiti cha urais,
Rais Goodluck Jonathan wa chama tawala cha PDP na Muhammud Buhari kutoka chama cha upinzani cha APC

na ambaye katika miaka ya nyuma amewahi kuwa kiongozi wa nchini hiyo wakati wa utawala wa kijeshi wanachuana vikali kuwania kiti hicho.

Saturday, 28 March 2015

Mtandao wa tume ya uchaguzi Nigeria warekebishwa


Hatimaye mtandao wa tume ya uchaguzi nchini Nigeria umeanza tena kufanya kazi

Mtandao wa tume ya uchaguzi nchni NIgeria INEC ambao ulikuwa umeingiliwa na kundi la wahalifu wa mtandao linalojiita jeshi la mtandaoni la Nigeria hatimaye umeanza tena kufanya kazi.
Kundi hilo linalojiita Jeshi la mtandaoni la Nigeria liliweka ujumbe katika tovuti hiyo likiionya tume ya uchaguzi ya Nigeria dhidi ya kufanya udanganyifu katika uchaguzi huo.
kufikia sasa haijulikani iwapo wahalifu hao wameingia zaidi ya mtandao huo ijapokuwa wamesema kuwa walikuwa wakithibiti data yote ya tume ya uchaguzi.
Tume hiyo imesema kuwa ina maelezo kuhusu shambulizi hilo la mtandaoni na sasa imeanza kufanya uchunguzi.
Ujumbe huo wa wahalifu hao wa mtandaoni pia unasema kuwa wameweza kuingilia data ya serikali.
Mitandao kadhaa maarufu ya serikali ya Nigeria imefungwa katika miaka ya hivi karibuni ukiwemo ule wa bunge.

Kutafuna ubani ni haramu, wapi huko ?

Moja ya sababu ambayo singapore iliharamisha utafunaji wa ubani

Wengi wanamkumbuka kiongozi muanzilishi wa Singapore Lee Kuan Yew,aliyeaga dunia jumatatu iliyopita akiwa na umri wa miaka 91.
Hata hivyo wengi wetu ambao hatuzuru Singapore hatujui anachosifiwa kiongozi huyo ila tu sifa kedekede anazolimbikizwa katika vyombo vya habari.
Hata hivyo mojawepo ya sifa hizo ni usafi.
Kiongozi huyo aliyeongoza kisiwa cha Singapore punde kilipopata uhuru wake yapata miaka 50 hivi iliyopita alipenda taifa hilo ambalo kimsingi ilikuwa ni
bandari igeuke na kuwa taifa huru linajitegemeakiuchumi.

Na si Hayo tu Lee Yew alitaka raia wa Singapore kujivunia taifa lao japo lilikuwa changa kiuchumi ikilinganishwa na jirani zake India China Japan na Korea

Rais Obama anauraibu wa kutafuna ubani

Hata ilipowadia zamu ya ustaarabu na usafi , Lee aliharamisha utafunaji wa ubani , na pipi zilizokuwa na kiungo kama raba kisa na maana ?
Yew alichukia sana watu waliotafuna ubani kisha wanatupa mabaki yake sakafuni pindi utamu wake unapokwisha.
Shinikizo la watu lilimfanya kuruhusu utafunaji wa ubani mwaka wa 1992 kwa muda kulingana naye kwa sababu vyombo vya habari vya kigeni vilikuwa
vinaangazia tu marufuku yake na kuwa watu walikuwa wanatandikwa viboko kwa makosa madogo madogo kama vile kutupa taka kukojoa hovio kutema

makohozi na makosa mengine kama hayo.

Muanzilishi wa Singapore Lee Kuan Yew,aliyeaga dunia jumatatu aliharamisha utafunaji wa big G

Marufuku hiyo ni moja ya maswala yanayangaziwa kwa kiasi kikubwa miongoni mwa wageni katika taifa hilo lililoshamiri katika ukuaji wake wa kasi wa uchumi na pato la nchi duniani.
Nichini Singapore, ni hatia kutembea ovyo,kuandika ukutani ,kutema makohozi kukojoa sehemu yeyote ile ila chooni.
Ukishatumia choo ni sharti umwage maji la sivyo utashtakiwa.
Hatua iliyopiga katika kipindi cha uhuru wake (tangu mwaka wa 1965) hadi sasa unazidi mataifa mengi yaliyokuwa na uwezo na rasili mali inayoizidi.
Chini ya uongozi wake Singapore ilikuwa inayazidi mataifa yaliyostawi kwa usafi wa miji na mazingira kwa jumla .
Lee ambaye alisomea chuo kikuu cha Camridge nchini Uingereza aliwalazimu raiya wa Singapore kutekeleza hali ya juu ya usafi.
Kulingana na rais Yew watu ambao walidai kuwa hawawezi kufikiria bila ya kutafuna tafuna aliwashauiri kutafuna ndizi.

LKY alisema kuwa japo wanakejeliwa kuwa'' taifa linaloshikilia kukutu usafi wa mazingira kama vile yaya na mtoto''

Mwili wa aliyekuwa kiongozi wa Singapore LKW

Singapore ilikuwa inafululiza katika ustawi wa kiuchumi bila ya kujali kejeli na matusi kuwa alikuwa ni dikteta.
Lee aliwadharau sana watu walikuwa wakitafuna ubani na pipi akisema kuwa wengi wao walikuwa watundu.
LKW alidai kuwa milango ya treni za umeme zilikuwa zinakwama kwa sababu mabaki ya ubani yalikuwa yanafichwa nyuma ya milango na hivyo kusababisha
kucheleweshwa kwa usafiri wa watu wenye bidii na ari ya kufika makazini mapema.
LKW alikerwa sana na tabia hiyo ndiposa akaamrisha imegwe marufuku kutokana na kinyaa na kero kwa hali ya usafiri na usafi wa Singapore.
Tafakari hayo ya LKW ,je yanawezekana katika mataifa yetu ya Afrika ?

Mtandao wa tume ya uchaguzi waingiliwa

Mtandao wa tume ya uchaguzi nchini Nigeria waingiliwa

Huku mamilioni ya raia wa Nigeria wakipiga kura kumchagua rais mpya,tovuti ya tume ya uchaguzi nchini Nigeria imeingiliwa na wahalifu wa mtandaoni.

Kundi linalojiita Jeshi la mtandaoni la Nigeria limeweka ujumbe katika tovuti hiyo likiionya tume ya uchaguzi ya Nigeria dhidi ya kufanya udanganyifu katika uchaguzi huo.
kufikia sasa haijulikani iwapo wahalifu hao wameingia zaidi ya mtandao huo ijapokuwa wamesema kuwa walikuwa wakithibiti data yote ya tume ya uchaguzi.
Tume hiyo imesema kuwa ina maelezo kuhusu shambulizi hilo la mtandaoni na sasa imeanza kufanya uchunguzi.
Ujumbe huo wa wahalifu hao wa mtandaoni pia unasema kuwa wameweza kuingilia data ya serikali.

Mitandao kadhaa maarufu ya serikali ya Nigeria imefungwa katika miaka ya hivi karibuni ukiwemo ule wa bunge.

PERFECT: Je utanunua simu iliyotengezwa na Nyasi ?

PERFECT: Je utanunua simu iliyotengezwa na Nyasi ?: Je utanunua simu iliyotengezwa na Nyasi ? Watu wengi wamekuwa wakilalamikia teknolojia na ufundi wa simu nyingi za kisasa wengi wakiwapond...

Matatizo ya kiufundi yaathiri uchaguzi

Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan akiongoea na wanahabari baada ya kushindwa kujisajili kutokana na sababu za kiufundi zinazokabili vifaa vya uchaguzi

Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan akiongoea na wanahabari baada ya kushindwa kujisajili kutokana na sababu za kiufundi zinazokabili vifaa vya uchaguzi

Mwandishi wa BBC nchini Nigeria anasema kuwa matatizo yameibuka kwenye vifaa vya mkononi ambavyo hutumiwa kusoma kadi za kupigia kura.
Rais Goodlack Jonathan ni miongoni mwa watu walioathiriwa na tatizo hilo swala lililomfanya usubiri nje ya kituo cha kupigia kura kwa mda.
Pia kuna ripoti za kutimuliwa kwa waangalizi kutoka kwa vituo vya kupigia kura na maafisa wa chama tawala.

Rais Jonathan anakabiliwa na upinzani mkali kutoka aliyekuwa kiongozi wa utawala wa kijeshi Muhammadu Buhari.

Je utanunua simu iliyotengezwa na Nyasi ?

Je utanunua simu iliyotengezwa na Nyasi ?

Watu wengi wamekuwa wakilalamikia teknolojia na ufundi wa simu nyingi za kisasa wengi wakiwaponda wabunifu kwa misingi ya kuwa

asilimia kubwa ya simu za mfumo wa 3G na zaidi zinatengezwa kwa plastiki.
Sasa basi,bwana mmoja mbunifu amekuja na jibu ya kutengeza simu kutokana na ''Nyasi'' .
Bwana Sean Miles amezindua simu itakayokuwa ya kipekee.

Simu hiyo ndiyo ya kwanza kuwahi kutengenezwa kwa asilimia 100% kutokana na bidhaa hai.
Gamba la juu la simu hiyo limeundwa kwa bidhaa inayotokana na nyasi maalum iliyochanganywa na kemikali fulani na kiungo (resin)
"mchanganyiko huu maalum unatoa sura kama vile (carbon) alisema Miles.
Mfumo huo unachanganywa na kumbwa kwa njia itakayoruhusu watengezaji wa simu kuumba gamba la simu inayotokana na nyasi.

Simu nyingi za kisasa hazina ubunifu na zinaelekea kufanana

Bwana Miles alikuwa amepewa kandarasi na kampuni ya simu ya O2 kutafuta mbinu ya kutumia upya bidhaa ambazo zimekosa wateja ama zimezeeka.
Hata hivyo kitengo cha ubunifu kilitamaushwa na ubunifu wake na sasa kimeanza mikakati ya kutathmini uwezo wa kampuni hiyo kuunda kwa wingi magamba ya simu.
Kufikia sasa asilimia 25% ya simu nzee nchini uingereza zinarekebishwa na kutumiwa upya.

Saudia yawaondoa raia wake Yemen kusini

Mji wa kusini wa bandari ya Aden nchini Yemen

Vyombo vya habari nchini Saudi Arabia vinasema kuwa nchi hiyo imewahamisha raia wake na wanadiplomasia wa kigeni kutoka mji wa bandari ya Aden kusini mwa Yemen.
Jeshi la wanamaji la Saudi Arabia liliongoza oparesheni hiyo.

Kundoka kwa watu hao kunajiri wakati waasi wa Houthi wanazidi kuelekea mji wa Aden.
Saudi Arabia iliongoza mashambulizi ya siku tatu dhidi ya waasi hao wanaoungwa mkono na Iran lakini hayo yote yameshindwa kuwazuia kusonga mbele

Wakaazi wameeleza kuwepo kwa mashambulizi makubwa ya angani kwenye mji mkuu wa Yemen, Sanaa.

Saudia yawaondoa raia wake Yemen kusini

Mji wa kusini wa bandari ya Aden nchini Yemen

Vyombo vya habari nchini Saudi Arabia vinasema kuwa nchi hiyo imewahamisha raia wake na wanadiplomasia wa kigeni kutoka mji wa bandari ya Aden kusini mwa Yemen.
Jeshi la wanamaji la Saudi Arabia liliongoza oparesheni hiyo.
Kundoka kwa watu hao kunajiri wakati waasi wa Houthi wanazidi kuelekea mji wa Aden.
Saudi Arabia iliongoza mashambulizi ya siku tatu dhidi ya waasi hao wanaoungwa mkono na Iran lakini hayo yote yameshindwa kuwazuia kusonga mbele
Wakaazi wameeleza kuwepo kwa mashambulizi makubwa ya angani kwenye mji mkuu wa Yemen, Sanaa.

Makabiliano Hotelini Somalia yamalizika


Makabiliano kati ya vikosi vya serikali na wapiganaji wa Al Shabaab katika hoteli ya Al Mukarama yamemalizwa kwa mujibu wa maafisa wa serikali ya Somalia

Maafisa wa serikali ya Somalia wanasema kuwa mapigano yalikuwa kwenye hoteli moja mjini Mogadishu kufuatia uvamizi wa wanamgambo wa Al shabaab yamemalizika.

Maafisa hao walisema kuwa wanajeshi wa serikali waliingia eneo hilo kuidhibiti hoteli ya Maka al Mukarama zaid ya saa 12 baada ya wanamgambo kuivamia.
Watu 9 waliuwa wakati wa uvamizi huo akiwemo mjumbe mmoja wa Somalia.
Waandishi wa habari eneo hilo wanasema kuwa miili ya wanamgambo na ya wanajeshi ilikuwa eneo hilo.
Wataalamu wa kutegua mabomu wanasaka hoteli hiyo kujua iwapo kuna milipuko yoyote.

Friday, 27 March 2015

Je,antibiotics husababisha kisukari?

Dawa za antibiotics

Wagonjwa wanaotibiwa na dawa za viuavijasumu ama antibiotics mara kwa mara huenda wakakabiliwa na hatari ya kupatwa na aina ya pili ya ugonjwa wa kisukari ,watafiti wamegundua.

Utafiti uliochapishwa na Jarida la utafiti wa damu ulifuatilia dawa zinazopewa mamilioni ya wagonjwa nchini Uingereza.
Waanzilishi wa utafiti huo wanasema kuwa matokeo ya utafiti huo hayamaanishi kwamba dawa hizo husababisha kisukari ,na badala yake maambukizi huenda ni ishara za mapema kwamba mtu anakabiliwa na kisukari.

Wanasema kuwa kazi ya ziada inahitajika ili kuelewa uhusiano huo.

antibiotics

''Ni utafiti mkubwa na wenye usaidizi unaohusisha kisukari na utumiaji wa dawa za viuavijasumu miongoni mwa wakaazi wa Uingereza,lakini kufikia sasa hatujui ni kipi kilichokuja mwanzo,ni kuku ama ni mayai yake'',professa Jodi Lindsay wa chuo cha St Georges mjini London alisema.
Utafiti huo uliangazia idadi ya dawa hizo zilipewa wagonjwa 208,000 wa kisukari cha aina ya kwanza na ya pili mwaka mmoja kabla ya kupatikana na ugonjwa huo ikilinganishwa na watu 816,000 wasio na ugonjwa huo walio na umri sawa na jinsia sawa.



Karibia nusu ya wagonjwa hao walipewa dawa hiyo wakati mmoja huku utafiti huo ukiendelea.
Watafiti walibaini kwamba hatari ya aina ya pili ya kisukari ilipanda juu kutokana na idadi ya dawa za viuavijasumu waliopewa.


Alshabab yaua watu 10 hotelini Somalia

Wapiganaji wa kundi la wanamgambo wa Al Shabaab wameshambulia mkahawa mmoja mjini Mogadishu na kua watu 10

Kundi la wapiganaji linaloshukiwa kuwa sehemu ya wanamgambo wa Al Shaabab , limevamia hoteli moja katika mji mkuu wa Somalia Mogadishu.

Wanajeshi wa serikali ya Somali wanaendelea kupambana na wanamgambo hao waliojihami kwa vilipuzi na bunduki za rashasha.
Watu 10 wameripotiwa kuuawa katika uvamizi huu.
Kwa mujibu ya walioshuhudia wapiganaji hao wa Al Shabaab walishambulia hoteli ya Maka al-Mukarama mjini Mogadishu moja katia ya hoteli maarufu mjini humo ambayo inapendwa na wengi wa wafanyikazi wa kimataifa na mabalozi.
Aidha balozi wa Somalia nchini uswisi Yusuf Bari Bari alinusurika kifo baada ya kukwepa kupitia dirishani.

Watu 10 wameripotiwa kuuawa katika uvamizi hu

Kikosi maalum cha kupambana na uvamizi wa aina hiyo kinaendelea kukabiliana na wapiganaji hao ambao wanasemekana kuwa wamebanwa katika orofa ya juu ambapo sasa wanarusha grenedi na kufyatua risasi kwa yeyote anayeonekana kuwavizia.
Afisa wa Polisi anayeongoza operesheni hiyo meja Ismail Olow ameiambia shirika la habari la Reuters kuwa kati ya wavamizi 9 waliotekeleza mashambulizi haya 6 tayari wameshauawa.
Kundi la Al Shaabab limekuwa likitekeleza mashambulizi ya aina hii katika hoteli zinazosifika kuwa mahala pa burudani kwa wageni na viongozi mashuhuri serikalini.
Shambulizi hili la leo linafuatia lingine lililoanza kwa bomu yapata mwezi mmoja uliopita nje ya hoteli hiyo.

Nigeria:Jeshi laichukua ngome ya B Haram

Jeshi la Nigeria lauteka mji wa Gwoza

Jeshi la Nigeria linasema kuwa limeuchukua mji wa kazkazini mashariki wa Gwoza unaoaminika kuwa ngome kuu ya Boko Haram.

Ni katika eneo hilo ambapo wapiganaji wa Boko Haram walitangaza uongozi wa kiislamu na ni miongoni mwa miji mikuu iliotekwa na kundi hilo katika kipindi cha hivi karibuni.
Tangazo hilo linajri siku moja tu kabla ya uchaguzi mkuu nchini Nigeria unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.
Uchaguzi huo uliahirishwa kwa mda wa wiki sita ili kutoa fursa kwa jeshi la muungano wa mataifa kupata mda zaidi wa kukabiliana na Boko Haram.
Rais wa Chad,taifa ambalo ni miongoni mwa yale yaliyo na vikosi vyake amesema kuwa vikosi vya Nigeria havijajizatiti.

Rubani alikuwa na matatizo ya kiakili

Ajali ya ndegeAjali ya ndege

Viongozi wa mashtaka nchini Ujerumani wanasema kuwa wamepata ushahidi unaosema kwamba rubani wa ndege ya Ujerumani ilioanguka katika milima ya ALPS na kuwaua abiria 150 alikuwa amemficha mwajiri wake kuhusu ugonjwa anaougua.

Maafisa hao pia wamesema kuwa walipata kijikaratasi cha ugonjwa kilichokuwa kimekatwa ambacho kilimtaka rubani huyo kupumzika siku ya kuanguka kwa ndege hiyo.

Maafisa wa Polisi wa ujerumani

Hatahivyo hawakupata ujumbe wowote wa rubani huyo kutaka kujitoa uhai wake.

Vyombo vya habari nchini Ujerumani vimeripoti kwamba faili ya rubani Andreas Lubitz mwenye umri wa miaka 27 katika shirika la anga za juu imeonyesha kuwa Andreas alikuwa na matatizo ya akili na alitakiwa kufanyiwa ukaguzi wa mara kwa mara.


Andreas Lubitz

Ripoti nyengine ambazo hazijathibitishwa zinasema kuwa alilazimika kuchukua likizo ya miezi sita kutoka kwa mafunzo ya urubani kutokana na shinikizo la akili.

Thursday, 26 March 2015

Wagombea waahidi uchaguzi wa amani Nigeria

Wagombea wakuu wa uchaguzi nchini Nigeria rais Goodluck Jonathan wa Nigeria na Muhammud Buhari

Wagombea wawili wa uchaguzi wa urais nchini Nigeria wameahidi kufanyika kwa uchaguzi wa amani,na kuongezea kuwa wataheshimu matokeo ya uchaguzi ulio huru na haki.

Rais Goodluck Jonathan pamoja na mpinzani wake wa karibu Muhammadu Buhari,pia wamewataka wafuasi wao kuiga mfano huo.
Uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika siku ya jumamosi baada ya kuahirishwa mwezi uliopita.
Mwandishi wa BBC amesema kuna wasiwasi kuhusu iwapo tume ya uchaguzi imejianda kusimamia uchaguzi huo na iwapo shughuli hiyo itaafikia matarajio ya wengi.

Maharamia waziteka meli mbili za Iran

Maharamia wa Somalia wateka nyara Meli mbili za Iran

Kitengo cha Umoja wa Mataifa kinachoshughulikia mihadarati na Uhalifu kimesema kuwa maharamia wameteka meli mbili za Iran za kuvua samaki katika ufuo wa Somalia.

Utakeji huo ni wa kwanza kufaulu tangu mwaka 2012.
Ushikaji doria na matumizi ya walinzi wenye silaha umesaidia kupunguza uharamia katika ufuo wa Somalia, ambao awali ulikuwa ukishirikisha zaidi ya meli 200 kwa mwaka.
Umoja wa Mataifa unasema kuwa wafanyakazi 48 wametekwa nyara katika uharamia huo.
Taarifa hiyo inasema kuwa meli hizo, zilizokuwa zikivua samaki bila kibali katika fuo hizo za Somalia zimepelekwa katika kijiji cha Pwani cha El Huur katikati mwa Somalia.
Ingawa uharamia ulikuwa umepunguka, idadi ya wavuvi haramu imeongezeka.
Uvuvi haramu ndio ulioanzisha mtindo wa kuteka meli Somalia.
Umoja wa Mataifa umeonya kuwa iwapo meli za kigeni zitaendelea kuvua samaki kimagendo katika ufuo wa Somalia, visa vya uharamia navyo vitaongezeka.

Ndege ya Ujerumani iliangushwa makusudi

Rubani Andreas Lubitz

Rubani wa ndege ya kampuni ya Germanywings ilioanguka katika milima ya Alps nchini Ufaransa siku ya jumanne alitaka kuiharibu ndege hiyo kulingana na maafisa wa Ufaransa.Kiongozi wa mashtaka katika mji wa Mersaille ,Brice Robin, akizungumza kulingana na habari aliyopata katika kijisanduku cha kunasa sauti katika ndege amesema kuwa rubani huyo alikuwa ndani ya chumba cha kuendesha ndege pekee.

Rubani huyo kimakusudi aliishusha ndege hiyo kwa kasi huku rubani mwenza akiwa nje ya chumba hicho cha kuendesha ndege.
Bwana Robin amesema kuwa kulikuwa na kimya kikubwa ndani ya chumba hicho wakati rubani mwenza alipojaribu kuingia kwa nguvu.

Hatahivyo abiria walisikika wakipiga nduru kabla ya kuanguka kwa ndege hiyo,aliongezea.
Mlima wa Alps ambapo ndege ya abiria ya Germanywings ilianguka

Rubani huyo kwa jina Andreas Lubtiz,mwenye umri wa miaka 28, alikuwa hai hadi wakati ndege hiyo ilipoanguka ,kiongozi wa mashtaka alisema.
Ndege hiyo aina ya Airbus 320 iliokuwa ikitoka Barcelona kuelekea Duesseldorf Ujerumani iligonga mlima na kuwauwa abiria wote 144 pamoja na wafanyikazi sita wa ndege baada ya kushuka kwa dakika nane.

"Tunasikia rubani akimuuliza rubani mwenza kuchukua udhibiti wa usukani wa ndege hiyo na vilevile tunasikia sauti ya kiti kikisonga nyuma na mlio wa mlango ukifungwa,bwana Robin aliwaeleza wanahabari.

RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA ATEUA WABUNGE WAPYA

Tokeo la picha la JAKAYA
 Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete,

Rais wa Jamhuri ya Muunganoi wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewateua wabunge wawili(2) wapya wa Bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Walioteuliwa ni Dkt. Grace Khwaya Puja na Bwana Innocent Sebba.

Rais amefanya uteuzi huu kw amamlaka aliyopewa na Katiba ya Jamhuri ya Muunganno wa Tanzania, ibara 66 (l) (e) ambapo amepewa mamlaka ya kuteua wabunge wasiozidi kumi (10).  Uteuzi huu umekamilisha idadi ya wabunge ambao Mheshimiwa Rais amepewa kwa mujibu ya mamlaka aliyonayo kikatiba.

Wabunge ambao wameteuliwa ni ;
Mhe. Profesa Makame Mnyaa Mbarawa
Mhe. Profesa Sospeter Mwijarubi Muhogo
Mhe. Dkt Asha Rose Migiro
Mhe. Janet Zebedayo Mbene
Mhe. Saada Salum Mkuya
Mhe. Zakhia Hamdani Meghji
Mhe. Shamsi Vuai Nahodha
Mhe. James Fransis Mbatia

UTAFITI UMEONYESHA ASILIMIA KUBWA YA VIJANA WA KITANZANIA WAMEHARIBIKIWA MAISHA SABABU YA BANGI


Kijana aliyeharibikiwa sababu ya bangi

Ford kuuza magari ya kusoma ishara

Gari la kampuni ya Ford
Kampuni ya magari ya Ford itaanza kuuza magari ambayo yatakuwa na uwezo wa kusoma ishara za barabarani na kurekebisha mwendo wake ili kuhakikisha kuwa gari haliendi kwa kasi.
Teknolojia hiyo inatumika kwa kutumia usukani wa gari na inaweza kutolewa kwa kutumia kikanyagio cha kuendesha gari iwapo dereva atakanyaga kikanyagio hicho cha mafuta kwa nguvu.
Kampuni hiyo ya magari inapendekeza kwamba kifaa hicho kitawasaidia madereva kukwepa kulipishwa faini na pia huenda kikapunguza idadi ya ajali.
Hatahivyo mtaalam mmoja amesema kuwa teknolojia hiyo itatumika kwa mda mfupi.
''Kuna mpango wa kudhibiti kasi ya gari lako kupitia kifaa kitakachowekwa katika kompyuta ya gari hilo na kudhibitiwa kutoka eneo hilo,badala ya kutafuta kifaa cha kusoma ishara za barabarani'',alisema Paul Newton mshauri wa maswala ya magari.

''Hii ni miongoni mwa mikakati itakayounganisha mifumo ya magari ,na kuyafanya magari kuonya magari mengine yalio nyuma yao iwapo yanataka kupunguza mwendo ikiwa ni kati ya mipango ya kutengeza magari yanayoweza kujiendesha.

PERFECT: Ajali ya ndege ''Rubani moja alifungiwa Nje''

PERFECT: Ajali ya ndege ''Rubani moja alifungiwa Nje'': Uchunguzi wa awali wa sauti zilizokuwa ndani ya kifaa cha kurekodia sauti ya ndege iliyoanguka Ufaransa unaonesha kuwa moja wa marubani wa n...

PERFECT: Mabibi harusi wa zamani Zimbabwe waongea

PERFECT: Mabibi harusi wa zamani Zimbabwe waongea: Raisi wa Zimbabwe Robert Mugabe Mabibi harusi wa zamani wawili wameamua kuipeleka serikali ya Zimbabwe mahakamani katika harakati za kuvun...

Mabibi harusi wa zamani Zimbabwe waongea

Raisi wa Zimbabwe Robert Mugabe

Mabibi harusi wa zamani wawili wameamua kuipeleka serikali ya Zimbabwe mahakamani katika harakati za kuvunja sheria kandamizi nchini humo na kutaka sheria inayoruhusu mabinti kuolewa wakingali wadogo iwe ni kinyume na katiba na si halali kwa kifupi iharamishwe.

Mabibi harusi hao Loveness Mudzuru na Ruvimbo Tsopodzi wamesema ndoa za utotoni ,ambazo ni ruksa nchini Zimbabwe,wansema ni sawa na ukatili wa kijinsia kwa watoto ambao huwanasa mabinti na kuishia katika janga la umasikini na madhila yasiyosemeka.
Nimekabiliana na changamoto zisizosemeka ,mume wangu alikuwa akinipiga sana.nilikuwa natamani kuendelea na masomo lakini yeye alikataa.nilikuwa na hali mbaya sana huu ni ushuhuda wa Tsopodzi, mama wa mtoto mmoja,mama huyu aliolewa akiwa na umri wa miaka kumi na mitano tu .
Na anaendelea kusema kwamba anataka kuchukua hatua hiyo ili kuleta tofauti,ameeleza hayo akiwa katika mji mkuu wa nchi hiyo Harare mapema wiki hii.Na hii yote ni katika harakati za kuzuia mabinti wadogo wanaoolewa katika umri mdogo.
Takwimu zilizochapishwa mwaka wa jana zinaonesha kwamba moja ya tatu ya wasicha walio na umri wa chini ya miaka kumi na nane huolewa , wakati wengine wapatao asilimia tano huolewa kabla ya kutimiza umri wa miaka kumi na mitano.
Katika tamko lao kwa mahakama ya katiba, Tsopodzi na Mudzuru, ambao kwa sasa wana miaka 19 na mwingine ana miaka 20, wanasema kwamba sheria ya ndoa nchini Zimbabwe ni ya kibaguzi kwani inamtaka mtoto wa kike aolewe akiwa na umri wa miaka kumi na sita wakati mtoto wa kiume anatakiwa kuoa akishatimiza umri wa miaka kumi na nane, na ndoa za kimila hazijaainisha umri halisi wa kijana ama binti kuoa ama kuolewa.
Sheria ya ndoa ya mwaka 2013 inasema kwamba kila mtoto mwenye umri wa miaka kumi na mitatu,anayo haki ya kupata malezi ya wazazi,elimu na ulinzi kutoka kwao katika masula ya unyonyaji kingono na kiuchumi.
Sheria hii pia haijaweka wazi umri wa kuoa ama kuolewa lakini inasisitiza kwamba hakuna mtu yeyote atakayelazimishwa kuoa ama kuolewa kinyume na matakwa yao na kuonesha wazi kuwa raia wa Zimbabwe mwenye umri wa miaka kumi na nane anaweza kuwa na familia yake.
Umasikini ndio chanzo cha ndoa za utotoni nchini Zimbabwe na kuwasababisha kuolewa kabla ya umri wao wasichana walio wengi ,na hivyo kuwasababisha wazazi kupunguza mzigo wa familia katika masuala ya matunzo na kubakisha mama tu na baba.ulipwaji mahari nayo ni motisha inayowafanya wazazi kutowatendea haki watoto wao.
Baadhi ya familia nchini Zimbabwe zinatukuza ndoa za utotoni kwa mtazamo wa kuwalinda watoto wao wa kike na ngono kabla ya ndoa.
Mudzuru anatoa ushuhuda wake kwamba ndoa za utotoni ni chagamoto kubwa ,kwani mabinti hao walio katika umri mdogo watazaa watoto wakiwa katika familia masikini na hapo ndipo mzunguuko wa ndoa za utotoni unapoanza upya.
Mudzuru, aliolewa akiwa na umri wa miaka kumi na sita kwa sasa ana watoto wawili tena akiwa hajatimiza miaka kumi na nane ,anasema maisha yake yalikuwa sawa na jehanamu ya moto na aliishi maisha yake katika dhiki isiyosemeka.
Nasema maisha yake yalikuwa magumu sana, kulea watoto ilhali wewe mwenyewe ukiwa ni mtoto ni vigumu,na asema katika umri wake alipaswa kuwa anahudhuria masomo shuleni.
Naye mwanasheria wa mabinti hao ambao ni akina mama sasa hivi,alikuwa ni waziri wa zamani wa fedha nchini humo Tendai Biti, aliwasilisha changamoto hizo za kisheria mwezi January mwaka huu.
Beatrice Savadye,yeye ni mwanaharakati wa kupinga ndoa za utotoni nchini humo anayeongoza asasi isiyokuwa ya kiserikali,ijulikanayo kaka ROOTS ,asasi ambayo inawaunga mkono akina mama hao wawili anasema kesi hiyo imekuwa na mvuto wa kipekee nchini humo nan je ya nchi hiyo kwa ujumla wake.

Na anamashaka kama mahakama itatoa maamuzi yake lini ,lakini inalazimika kutoa maamuzi yake ndani ya miezi sita.
Wazimbabwe
Ulimwenguni kwa ujumla wake wasichana milioni kumi na tano wanaolewa kila mwaka.katika jangwa la sahara peke yake asilimia arobaini ya wanawake huolewa wakiwa katika umri mdogo.

Ajali ya ndege ''Rubani moja alifungiwa Nje''

Uchunguzi wa awali wa sauti zilizokuwa ndani ya kifaa cha kurekodia sauti ya ndege iliyoanguka Ufaransa unaonesha kuwa moja wa marubani wa ndege hiyoalikuwa amefungiwa nje ya eneo la marubani wakati ndege hiyo ilipoanguka.

Aidha haijabainika kikamilifu alikuwa ameondoka kufanya nini lakini sauti zinasikika akibisha kwa nguvu akitaka ufunguliwe mlango.
Duru za kuaminika zinanukuliwa na jarida la New York Times.
Mkuu wa shirika la ndege la Lufthansa amesema kwa kinywa wazi kuwa kuanguka kwa ndege hiyo kuna hila hila.
''hakuna maelezo kamili ya kiini cha ajali hiyo ''

''Ndege hiyo ilikuwa imefanyiwa ukarabati majuzi tu wala haikuwa na hitilafu yeyote''.
nini kilitokea? swali halina jibu,kisanduku cheusi kimeharibika
Wakaguzi wa kifaransa wamesema wamefanikiwa kukipata kifaa cha kurekodia sauti na maneno kutoka katika kisanduku cheusi cha ndege ya shirika la ndege la ujerumani iliyopata ajali katika milima ya Alps.
Wakaguzi hao mpaka sasa wanaendelea kukitafuta kisanduku kingine ,ambacho hurekodi taarifa za ndege hiyo na chanzo cha ajali hiyo .
Timu hiyo ya uokozi iliyoko katika eneo la ajali lililoko upande wa Kusini mwa Ufaransa wamefanikiwa kukipata kifaa hicho kinachohifadhiwa katika chumba cha rubani kikiwa kimeharibika.
David Gleave ni mkaguzi wa zamani wa ajali za ndege ,anasema kwamba visanduku hivyo vinapaswa kuwa na picha dhahiri za nini kilichotokea .
pengine tunaweza kupata mawasiliano ya timu ya wafanya kazi wa ndege hiyo,ambayo yatatuelekeza katika kilichojiri na chanzo cha tatizo ambalo walijaribu kulitatua pamoja kama timu,
na hatua walizochukua kunusuru janga hilo.

Je rubani alichukua juhudi za makusudi kuwanusuru abiria na wafanyakazi waliokuwemo

Je rubani alichukua juhudi za makusudi kuwanusuru abiria na wafanyakazi waliokuwemo,na rubani mwingine aliendelea kurusha ndege?
Ama kutatua tatizo?na namna walivyohakiki na nini walichokiacha na mambo kama hayo.
Hata hivyo tunahitaji zaidi taarifa za kinasa taarifa ili tuweze kupata mustakabali kamili wa kile kilichotokea.
Akizungumza katika mkutano na waandishi habari Carsten Spohr ambaye ni mkurugenzi mtendaji wa shirika la ndege la Germanwings shirika dada la kampuni ya usafirishaji ya Lufthansa ameielezea ajali hiyo kuwa isiyoeleweka.
niamini baada ya miaka ishirini ijayo katika tasnia hii nami niliwahi kuwa rubani wa shirika la ndege la Lufthansa,bado hainiingii akilini juu ya kile kilichotokea jana.

Mishumaa ya maombolezo ikiwashwa.
Shirika la ndege la Lufthansa halijawahi kupoteza ndege yake katika historia yake ya usafirishaji katika mazingira kama hayo ,bado
hatuelewi nini kiliisibu ndege iliyokuwa katika hali nzuri kiufundi na marubani wawili waliobobea katika kazi yao na waliopitia mafunzo ya hali ya juu ya safari za anga wa shirika la Lufthansa,kuhusika katika ajali mbaya kiasi kile .